Postedy by Esta Malibiche on August 27.2016 in News
Meneja
wa Buni Hub Jumanne Mtambalike akifafanua jambo katika Majadiliano
yaliyoratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) kwa
lengo la kujadili Ripoti ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016
iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni muongoza mada Amon Tamilwai. Jukwa hilo limekuwa likikutana
kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la
kujadili mada mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra.
Mratibu
wa Program kutoka Actuality Media Bi. Audrey Fancher akielezea jambo
katika Majadiliano yaliyoratibiwa na Jukwaa la Ujasiriamali Jamii
Tanzania (TASEF) kwa lengo la kujadili Ripoti ya Hali ya Ajira kwa
Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana
Jijini Dar es Salaam. Jukwa hilo limekuwa likikutana kila Ijumaa ya
mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la kujadili mada
mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra.
Baadhi
ya Vijana wakichangia mada katika Majadiliano yaliyoratibiwa na Jukwaa
la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF) kwa lengo la kujadili Ripoti ya
Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi
Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Jukwa hilo limekuwa likikutana
kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la
kujadili mada mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra.
Baadhi
ya washiriki wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF)
wakifuatilia mada katika Majadiliano kuhusu Ripoti ya Hali ya Ajira kwa
Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi Dunia (ILO) jana
Jijini Dar es Salaam. Jukwa hilo limekuwa likikutana kila Ijumaa ya
mwisho wa mwezi ambapo ukutanisha vijana kwa lengo la kujadili mada
mbalimbali zenye muelekeo wa kumkomboa kijana kifikra.
Baadhi
ya washiriki wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF)
wakibadilishana mawazo mara baada ya kumaliza Majadiliano kuhusu Ripoti
ya Hali ya Ajira kwa Vijana ya mwaka 2016 iliyotolewa na Shirika la Kazi
Dunia (ILO) jana Jijini Dar es Salaam. Majadiliano hayo yameratibiwa na
Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF).

ya waratibu wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF), kutoka
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa wa TASEF Adian Nzamba, Mratibu wa TASEF Bi.
Genoveva Emanuel Mtiti na Mshereheshaji Amon Tamilwai.
…………………………………………………………………….
Na: Frank Shija, MAELEZO.
Vijana
nchini wanatakiwa kujijengea mazoea ya kupenda kujifunza kila wakati
ili kuendelea kuibua mawazo endelevu kwa mustakabari wa maendeleo yao.
Hayo
yamesemwa na Rais wa Jukwaa la Ujasiriamali Jamii Tanzania (TASEF)
Adrian Nzamba wakati wa majadiriano ya Ripoti ya Hali ya Ajira
iliyoandaliwa naShirika la Kazi la Dunia (ILO) wakati wa majadiliano
yaliyoandaliwa na Jukwaa hilo jana Jijini Dar es Salaam.
“Vijana tunatakiwa tuwe na moyo wa kujifunza, wengi wetu wamekuwa wazito kujifunza” . Alisema Adrian.
Aliongeza
kuwa kupitia Jukwaa hilo wamekuwa wakiwajengea uwezo Vijana katika
hatua ya kujitambua na kuepukana na mawazo mgando yenye fikra hasi.
Kwa
upande wake Meneja wa Buni Hub mshiriki mwenza wa Jukwaa hilo Jumanne
Mtambalike ameipongeza Serikali kwa mchango wake katika kusaidia Vijana
kufikia malengo yao.
Mtambalike
amesema kuwa wao kama Buni Hub wamekuwa chini ya Tume ya Sayansi
Tanzania (COSTECH) ambayo ni Taasisi ya Serikali hivyo ni dhahiri kuwa
Vijana wakijitambua wanazo fursa nyingi kupitia Serikali yao kwani wao
kama taasisi binafsi lakini wananufaika.
Aliongeza
kuwa lengo kubwa la kushiriki Jukwa hilo ni kuwajengeauwezo vijana wa
kufikiri na kujitegemea badala kukaa na kulalamika bila sababu ya
msingi.
“Vijana
tumekuwa na tabia ya kulalamika sana, zipo fursa nyingi tu ili mradi
unapata taarifa tafuteni taarifa zipo fursa nyingi sana binafsi nilipata
udhamini wa kusoma nje ya nchi kupitia Wizara ya Habari kwa sababu
nilitafuta taarifa”. Alisema Mtambalike.
Aidha
alitoa rai kwa Taasisi za Elimu ya Juu kushirikiana na wadau mbalimbali
ili kuangaliana namna ya kuwa na njia bora ya kuwaandaa vijana ili
kukidhi mahitaji ya soko la ajira.
Katika
Jukwaa hilo vijana waliibua hoja mbalimbali zikiwemo kubadilisha mfumo
wa Elimu ili kuingiza mitaala ya Ujasiriamali, vijanga kujishughulisha
na utafutaji wa taarifa na msisitizo wa vijana kushiriki katika kazi za
kujitolea.
0 maoni:
Chapisha Maoni