Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akifunga mafunzo maalum ya
kupambana na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba la
Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori
kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika
kupambana na kukabiliana na majangili. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Balozi wa Marekani nchini
Tanzania, Mark Childress akizungumza wakati wa kufunga mafunzo maalumu
ya ya kupambana na ujangili kwa Askari wanyamapori katika Pori la Akiba
la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo hayo yatawasaidia Askari
wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu
katika kupambana na kukabiliana na majangili. ( Picha na Lusungu
Helela- MNRT)
Askari wanyamapori wakionesha kwa
vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu yaliyofanyika katika Pori la
Akiba la Rungwa Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna
ya kupambana na majangili wakati wakiwakamata majangili ( Picha na
Lusungu Helela- MNRT)
Askari wanyamapori wakionesha kwa
vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu yaliyofanyika katika Pori la
Akiba la Rungwa Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna
ya kupambana na majangili wakati wakiwakamata majangili ( Picha na
Lusungu Helela- MNRT)
Baadhi ya askari wanyamapori
waliohitimu mafunzo wakiwa kwenye paredi jana katika Pori la Akiba la
Rungwa mkoani Singida, Mafunzo hayo yatawasaidia Askari wanyamapori
kupata taarifa za kitenteligensia kwa ustadi wa hali ya juu katika
kupambana na kukabiliana na majangili. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa wanyamapori Tanzania ( TAWA) Childress akizungumza wakati
wa kufunga mafunzo maalumu ya ya kupambana na ujangili kwa Askari
wanyamapori katika Pori la Akiba la Rungwa mkoani Singida jana. Mafunzo
hayo yatawasaidia Askari wanyamapori kupata taarifa za kitenteligensia
kwa ustadi wa hali ya juu katika kupambana na kukabiliana na majangili.
( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
Askari wanyamapori wakionesha kwa
vitendo wakati wa kuhitimu mafunzo maalumu yaliyofanyika katika Pori la
Akiba la Rungwa Mkoani Singida yaliyohitimishwa jana wakionesha namna
ya kupambana na majangili wakati wakimkama ta jangili akiwa
amejisalimisha yeye mwenyewe. ( Picha na Lusungu Helela- MNRT)
…………………………………………………………………………
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ametoa wito kwa watu
wanaojihusisha na vitendo vya ujangili waache kazi hiyo baadala yake
watafute kazi nyingine zitakazoweza kuwaingizia vipato halali kwa
kufanya hivyo wataweza kujiepusha kutiwa nguvuni na askari wanyamapori
waliobobea kwa kazi hiyo.
Milanzi alitoa wito huo jana
wakati wa akifunga mafunzo maalumu ya kupambana na Ujangili kwa
askari wanyamapori katika pori la akiba la Rungwa mkoani Singida
yaliyofadhiliwa na Marekani na yaliyotolewa na Kikosi maalum cha
wanajeshi kutoka Marekani.
Amesema kuwa mafunzo hayo ni
muhimu sana kwa askari wanyamapori ili kuendelea na kukabiliana na
wimbi kubwa la ujangili kwa kuwa majangili wasasa wanatumia silaha za
kisasa tofauti na majangili wa zamani ambao walikuwa wakitumia upinde
na mishale.
Aliongeza kuwa majangili wa sasa
ambao askari wanyamapori wamekuwa wakikabiliana nao maporini ni wale
ambao wanatumia silaha za kivita hiyo ni lazima askari wetu wapewe
mafunzo ya hali ya juu ili waweze kukabiliana nao.
Aidha Katibu Mkuu, Milanzi alisema
Wizara imejipanga kuhakikisha suala la ujangili linakwisha ambapo kituo
kingine cha mafunzo ya kijeshi kwa askari wanyamapori cha Mlele
kilichopo Mkoani Katavi kimeanzishwa mbali na vyuo vya Pasiansi na
Mweka, Likuyu Sekamaganga ambavyo pekee ndivyo vilivyokuwa vikitoa
mafunzo kwa askari wanyamapori.
Aliongeza kuwa, kwa sasa Serikali
imejipanga kwa kushirikiana na Interpol kuhakikisha kuwa hatakamatwa
jangili tu aliyehusika kuua mnyama porini bali mtandao wote utakamatwa
na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria mahali popote.
Akizungumza na wahitimu wa mafunzo
hayo, Milanzi alisema mafunzo hayo yamejikita kuwasaidia kupambana na
majangili, magaidi pamoja na majambazi ambapo wao ndo watu wa kwanza
kukumbana nao wakiwa porini kwani ndiko wanakotumia kujificha kwahiyo
ujuzi walioupata umewaongezea ufanisi katika kulinda maliasili zilizopo
kwenye maeneo yao.
Aliwataka pia wahitimu hao kufanya
kazi kwa kujituma wasiishie tu kusherekea kumaliza mafunzo bali
waonyeshe kwa vitendo hii itasaidia na kuipa ari Marekani pamoja na
Asasi za kimataifa zenye lengo la kusaidia nchi katika vita dhidi ya
Ujangili.
Kwa upande wake Balozi wa
Marekani nchini Tanzania, Mark Childress amewataka wahitimu wazingatie
mafunzo waliyopata kwa kuyafanyia kazi ili Pori la Akiba la Rungwa liwe
sehemu salama kwa wanyamapori wanaopatikana katika pori hilo.
Ameahidi kuwa nchi yake itaendelea
kuisaidia Tanzania kwa kuwa suala la ujangili bado ni kubwa
linalohitaji ushirikiano wa pande zote ili liweze kutokomezwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni