Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akizungumza wakati wa ufunguzi wa
mkutano baina ya Wataalamu kutoka Jijini la Dar es Salaam na Madiwani
kutoka baadhi ya Halmashauri za Uganda Magharibi na Kaskazini wakati wa
ziara yao ya kujifunza masuala mbalimbali leo Jijini Dar es
Salaam.Kutoka kulia ni Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Majiji Tanzania
(TACINE) Bw. Philotheusy Mbogoro, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji
la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka ya Miji nchini Uganda
(UAAU) Mhe. Sanya Wilson.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa akielezea jambo wakati wa
ufunguzi wa mkutano baina ya Wataalamu kutoka Jijini hilo na baadhi ya
Madiwani kutkoka Halmashauri za Miji nchini Uganda wakati wa ziara yao
ya kujifunza masuala mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto
ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama
cha Mamlaka ya Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson na Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles
Afisa Uhusiano na Itifaki wa Jiji
la Dar es Salaam Gaston Mwakwembe akielezea jambo wakati wa mkutano
uliowakutanisha baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Jiji na baadhi ya
Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Madiwani hao
wapo katika ziara ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya
Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha na namna ya kuongoza
mabaraza ya Madiwani.
Mhandisi wa Barabara wa
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Swalehe Nyenye akiwasilisha maada
kuhusu mkakati wa kuboresha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam leo
wakati wa ziara ya baadhi ya Madiwani kutoka Uganda walipo nchini kwa
ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya Usafiri,
Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya
kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam Godhelp Ringo akifafanua maada kuhusu muundo wa
Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya baadhi ya Madiwani kutoka
Uganda waliopo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo
Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha
mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Baadhi ya Madiwani kutoka nchini
Uganda wakifuatilia mada kutoka kwa wataalamu wa Jiji la Dar es Salaam
wakati wa ziara kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Barabara
na Mitaa, Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu,
Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Baadhi ya Madiwani kutoka nchini
Uganda wakifuatilia mada kutoka kwa wataalamu wa Jiji la Dar es Salaam
wakati wa ziara kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Barabara
na Mitaa, Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu,
Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akimkabidhi zawadi Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji
nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya
Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni
Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip
Mwakyusa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akipokea zawadi kutoka kwa Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za
Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya
Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia
ni Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip
Mwakyusa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akimkabidhi zawadi Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji
nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya
Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni
Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip
Mwakyusa.
Picha na Frank Shija, MAELEZO.
0 maoni:
Chapisha Maoni