Mh.Lowasa akiendelea na mikutano ya ndani ya chama cha Democrasia na Maendeleo mkoani Njombe tarehe 23.8.2016 |
Ilula |
Iringa Mjini |
Mjumbe
wa kamati kuu na waziri mstaafu Edward Lowasa
akiendendelea na vikao vya ndani mkoani IRINGA tarehe 25.8.2016,akiwa mkoani Iringa
alitembelea kata Ilula na baadae kuhitimisha katika jimbo la Iringa
mjini ikiwa na lengo la
kukijenga chama katika maandalizi ya operation UKUTA september 1
Ilula |
Mbunge wa viti maalum chadema Mh.Risala Kabongo akiwa na diwani wa kata ya Ilula chadema Raymond Francis mara baada ya kumalizika kikao cha ndani Ilula |
WAZIRI Mkuu Msaafu aliyegombea urais kupitia Chadema na
kuungwa mkono na mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Edward Lowassa, amesema kuwa katika
uchaguzzi mkuu ujao atakwenda ikulu bila ya kumwaga damu ya mtu yoyote kwa kuwa
watanzania wanaimani naye.
Kauli hiyo aliitoa jana ilipowasili mkoani Iringa alipokwenda
kuzungumza na wafuasi wa chadema kwenye
vikao vyao ndani vinavyoendelea nchi nzima juu ya kampeni ya kupinga uvunjwaji
wa demokrasia nchini (UKUTA )
Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
alisema kuwa licha ya kwamba uchaguzi ulikwisha kupita lakini anaamni na watanzania wanaamini alishinda
kwa kura nyingi lakini aliamua kukaa kimya maana kila jambo linalotendeka mungu ana
makusudi nalo
“vijana wengi
hawakuridhika na vijana walinifuata na kuniambia twende tukadai haki yetu lakin
wataqnzania ndio walke wale tumeoleana sasa kuna haja gani mimi kwenda ikulu na
damu za watanzania mikononi sikutaka hilo lakini napenda kuwaambia 2020
tunakwenda ikulu kwa kuwa sababu ya kwenda ikulu tunayo
Sababu moja wapo ya sisi kwenda ikulu ziko nyingi moja maeneo
makubwa ya majiji wameshikilia wao na ndio maana anawataka madiwani wote walioko
katika maeneo hayo wafanye kazi kwa
bidii ili wasiwaangushe watanzania waliowaamini na kuwapa dhamana ya kuwaongoza
Chama cha mapinduzi kimejeruhiwa ndio maana wanahangaia
kuzuiya kila nifanyacho wananizuiya mimi
nilianza kufanya ziara zangu za kuwambia watanzania asante lakini ccm na serekali
yake wameamua kunizuiya kila niendeko ili niseme tu asante lakini nikenda huku polisi nikenda
kule polisi lakini natamani nimfikie
kila mmoja hata yule ambaye hakunipigia kura lakini aliniwazia mema nataka
nimfikie nimwambie asante lakini
wananizuiya sasa na nyie nawatuma kawambieni lowasa anasema asante sana .
Lowasa alisema kuwa sasa kazi iliyobaki ndani ya chama hicho
ili kuweza kushika dola ni mkuhimu kupenda kushirikiana kwa kila jambo
wafanyalo ili kuweza kujenga nguvu moja ya kulelekea ikulu kwa kuwa ninjiani
nyeupe na tayari mtimishi wa mungu Nabii Tibi Joshua alishamwambia kuwa
serekali ijayo ni serekali ya chadema hivyo hata yeyew anaamini kuwa itakuwa
hivyo
Hashim Juma Issa
kutoka Baraza la Wazee Taifa alisema
kuwa jambo wanalofanya la kupinga uvunjwaji wa demokrasia nchini hawabahatishi
na wala hawatishi watu bali watatekeleza
dhamira yao kwa kuwa wanataka haki itendeke ndani ya nchi bila ya kuvunja
katiba ya nchi .
Alisema kuwa Amani na utulivu wa watanzania iko mikononi mwa
watanzania wenye na wala haiko mikononi mwa chama chochote hivyo ni vyema vyama
vya siasa vikaheshimu maamuzi ya watanzani na kuwapa uhuru wa demokraisa bila
ya kuwatisha na kuvunja katiba ya nchi .
“Siku hiyo ikifika ya sepetember
1 niwaombeni wote fanyeni maandamano yenu kwa Amani na utulivu
bila ya kufanya vurugu yoyote wala kugusa gari ya mtu wala kikombe cha mtu kwa kuwa chadema ni watu wa Amani na sasa huu ni mtihani wetu wa kwanza tuwaonyesha
watanzania sisi sio watu wa vurugu bali tunataka haki etendeke bila ya
kupendelea upande wowote ”
0 maoni:
Chapisha Maoni