Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
Na Sheila Simba-MAELEZO
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa viongozi wakisiasa Nchini, kuwa
wavumilivu ili kulinda Amani ya Nchi.
Sheikh Alhad ameyasema hayo leo, ofisini
kwake, jijini Dar es Salaam ambapo amewataka viongozi hao kutii mamlaka iliyoko
kwani mamlaka hiyo imewekwa na Mungu na hivyo ni vema kutafuta njia nyingine
kumaliza matatizo yanapotokea.
“Ipo haja ya kuvumiliana kwa
ajili ya Taifa letu, kwani yanapotokea machafuko waathirika wakubwa ni
wanawake, watoto na vijana wetu ambao wanaweza kupata madhara makubwa na hata
kupoteza maisha’’alisema Alhad
Akizungumzia maandamano ya
ukuta yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi, amesema kuwa kauli ya kuzuia
maandamano hayo imetolewa na Rais wa Nchi na kuomba kauli hiyo kuchuliwa kwa
uzito wa kipekee, kwani busara ni kusikiliza mamlaka imesema nini na kutii
kauli hiyo ya Rais.
“Nawashauri Watanzania wenzangu, viongozi wangu wa kisiasa
jambo hilo si vyema tukashiriki kwani kutotii mamlaka ni dhambi ndivyo vitabu
vya dini vinanavyosema,’’ alifafanua Sheikh Alhad
Ameongeza kuwa suala la
kulinda amani ni la watanzania wenyewe kwa kusaidiana na Jeshi la Polisi ili
kuhakikisha amani inaendelea kuwepo, kwani ni rahisi kupoteza amani tuliyonayo
lakini ni vigumu kurudisha amani.
Amesema kuwa vijana
wasikubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine kwani kufanya hivyo ni
kushindana na dola na kutolea mfano wa machafuko yanayoendelea kwa baadhi ya
Nchi Duniani na kupelekea mataifa hayo kutokalika kutokana na vurungu za
kisiasa.
Aidha amewaomba vijana
kutokubali kulitia doa Taifa, kwani Tanzania inafahamika ni kisiwa cha Amani
Duniani na inapaswa kulinda heshima hiyo ili kuendelea kutunza amani ya Watanzania
wote bila kujali tofauti za kisiasa.
0 maoni:
Chapisha Maoni