Postedy by Esta Malibiche on August 17.2016 in SIASA with No comment
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU CCM TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Katibu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Siraji Madebe |
Kimeazimia yafuatayo:-
Kuunga mkono utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kwa kuelimisha wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM taifa Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu umuhimu wa kila mwananchi kudai risiti na muuzaji kutoa risti katika kila manunuzi, kwa lengo la kuwezesha serikali kupata fedha kupitia kodi, kutoa elimu kwa jamii na uelewa wa Tanzania yenye viwanda ikiendana na uwanzishaji wa mashamba darasa ya shirikisho na viwanda vya kati vya kusindika mazao.
Vilevile
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, tunafungua milango kwa
vijana mbali mbali wenye lengo la kuunda vikundi vyenye dhamira ya
kujikwamua kiuchumi na kutaka kujiajili, kufika kwenye ofisi zetu za
Shirikisho zilizopo mikoani na Makao Makuu, mtaa wa Lumumba jijini Dar
es Salaam, ili kupata ushauri wakitaalamu na kusaidiwa kuandika maandiko
yatakayo waongoza kwenye uanzishwaji wa miradi itakayo saidia kutoa
fursa za ajira kwa vijana.
Pia
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, linamuomba Mwenyekiti wa
CCM, Rais Dk. John Magufuli, kuwashughulikia kikamilifu wale wote
waliohujumu mali za CCM, kwani vitendo hivyo vinadhoohofisha nguvu ya
chama na wakati mwingine kuwafanya wanachama kuwa wanyonge kwenye Chama
chao.
Shirikisho
la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, kwa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM,
kwa kuhamia Dodoma, tumeazimia kuwa Ofisi ya Makao Makuu ya Shirikisho
nayo itahamia Dodoma rasmi hivi karbuni, baada ya taratibu za
upatikanaji wa Ofisi kukamiliaka.
Mwisho,
Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, linapenda kuwaomba Watanzania
kuendelea kumuunga mkono na kumuamini kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Pombe Magufuli
kwani dhamira yake ni kuitumikia jamii ya Watanzania na si kufanya siasa
kwenye maisha ya watu wenye shida.
KUDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:-
Idara ya Habari na Mawasiliano
Shirikisho Makao Makuu
0 maoni:
Chapisha Maoni