Postedy by EstaMalibiche on August 26.2016 in News
Na Sheila Simba,MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema kuwa
Rais Magufuli amedhamiria kuwatumikia wananchi na kuhakikisha maendeleo
yapatikani kwa Watanzania wote.
Akizungumza katika kipindi kipya
cha “TUNATEKELEZA” kinachoandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO na TBC1
Waziri Simbachawene alisema kuwa serikali ipo kwa ajili ya kufanya kazi
ya kuwatumikia wananchi katika kila sekta ili kutatua changamoto
zinazowakabili.
“Kupitia falsafa yetu ya hapa
kazi tu tutahakikisha tunawaletea wananchi maendeleo kutokana na ahadi
zilizoaidiwa kutoka katika ilani 2015-2020 ya Chama Cha Mapinduzi
kilicho na serikali.”
Alisisitiza kuwa Rais Magufuli
ameamua kuleta mabadiliko ya kweli hapa nchini ambayo yanalenga kuwabana
wabadhirifu wa mali za umma na kurejesha kurejesha nidhamu ya kazini
jambo ambalo limeanza kuonekana katika Ofisi mbalimbali za umma.
Waziri huyo amewahakikishia
wananchi kuwa ahadi za maendeleo zilizotolewa na Serikali ya awamu ya
tano zitatekelezwa kama ilivyopangwa kwani wanayo dhamira ya kweli ya
kuwatumikia wananchi.
Alisema kuwa suala la
kusimamiana kazini ni la kawaida na ni wajibu wa kila mtumishi hakikishe
anatimiza wajibu wake katika nafasi aliyopewa ili aweze kutekeleza
majukumu yake kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wa serikali kwa
kuweka uzalendo mbele.
Aliongeza kuwa ari na nidhamu ya
utendaji kazi mikoani imebadilika na watu wanafanya kazi kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora,kwani baadhi ya watumishi wa Halmashauri
walikuwa wanafanya kazi kwa mazoea.
Kuhusu watumishi hewa alisema
kuwa serikali imeondoa watumishi 12,000 waliokua wananchukua mishahara
bila kufanya kazi na kuomba wananchi kuunga mkono juhudi za serikali
katika hatua wanazochukua.
“upangaji mzuri wa watumishi
kwenye maeneo ya utoaji huduma kwa wananchi kwa maana ya Halmashauri
utakuwa umekaa vizuri kwa asalimia kubwa hata kwa kuwapanga vizuri bila
wafanyakazi hewa kuwepo”alifafanua Waziri Simbachawene
Alisema kuwa suala la wataalamu
wa fani mbalimbali kupendelea kubaki mijini ni tabia na kukosa uzalendo
kwani baadhi ya watumishi wanaopagiwa mikoani hawaripoti kutokana na
mazingira jambo ambalo sio sahihi.
“hata huku mijini wanakokimbilia
hakuna nyumba za watumishi basi imekuwa ni tabia tu ya watu kukosa
uzalendo”alisema Simbachawene.
0 maoni:
Chapisha Maoni