Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua Maabara ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu
wakati wa ziara yake hiyo ya kikazi hivi karibuni Agosti 2016.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kwa msimamizi wa Maabara ya
Hospitali ya Wilaya ya Kishapu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiwaonyesha namna wanavyokiuka taratibu za ndani ya
Maabara ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akihoji namna ya mpangilio wa Maabara unavyokosewa
na wasimamizi wa Maabara ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akielekeza namna ya Maabara inavyotakiwa iwe
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla (kulia) akitoa maagizo kwa Viongozi wa Serikali na
watendaji wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafanyia marekebisho mapungufu
yote yaliyobainika ndani ya miezi mitatu yawe yamepatiwa ufumbuzi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiagana na viongozi wa Hospitali ya Wilaya ya
Kishapu
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amezitaka Maabara Nchini kuhakikisha zinafuata
misingi na kanuni sahihi katika kuzingatia ubora na ufanyaji.
Akiwa
katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Shinyanga, Naibu Waziri wa Afya
Dk. Kigwangalla aliweza kukagua Maabara ya Hospitali ya Wilaya ya
Kishapu ambapo alibaini mambo mbalimbali yakifanywa bila kuzingatia
taratibu sahihi za Mabara huku akiagiza Mganga Mkuu wa Wilaya
kuhakikisha wanarekebisha mapungufu hayo katika Maabara hiyo.
Miongoni
mwa mambo ambayo alikuta katika Maabara hiyo ni pamoja na kutokuwa na
taratibu za kiutendaji hasa kwa wafanyakazi wenyewe wa Maabara ambao
walishindwa kuzingatia vigezo na msharti ambayo taratibu za Maabara
zinahitaji.
Picha na Andrew Charle
0 maoni:
Chapisha Maoni