Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yamepangwa usiku wa Alhamisi ya Agosti, 25 katika halfa ambayo inataraji kuambatana na kutangazwa kwa mchezaji bora Ulaya kwa mwaka 2016.
Kundi ambalo linaonyesha kuwavutia watu wengi ni kundi D ambalo lina timu za Barcelona, Manchester City, Borussia Monchengladbach na Celtic.
Sababu ya kundi hilo kuwavutia watu wengi ni kutokana na kumkutanisha kocha wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa anafundisha Manchester City, Pep Guardiola na hiyo ikiwa siyo mara ya kwanza kwa Pep kukutana na Barcelona akiwa na timu nyingine kwani hata alipokuwa Bayern Munich alikutana na Barca na kupokea kichapo ambacho kilimtoa nje ya mashindano.
Kundi lingine ambalo linaonekana kuwavutia watu wengi ni kundi A ambalo lina timu za PSG, Arsenal, FC Basel na Ludogorets Razgrad na jambo ambalo linaonekana kuwavutia watu wengi ni kutokana na uwepo wa Arsenal ambayo kwa sasa inaonekana haipo katika kiwango bora.
Ratiba kamili ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni;
Makundi UEFA