Postedy by Esta Malibiche on August 29.2016
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Iringa imemtangaza
Joseph Ryata (Chadema)kuwa mshindi halali wa kiti cha udiwani wa kata ya Kwakilosa katika Halmashuari ya
Manispaa ya Iringa baada ya kutupa hoja zilizofikishwa mahakamani hapo kupinga
ushindi huo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Makazi Mfawishi wa mahakama hiyo
David Ngunyale alisema upande wa mlalamikaji umesindwa kutoa ushahidi unaotosha
kuishawishi mahakama kutengua matokeo
hayo ya uchaguzi wa 2015 kama ulivyodai.
Hakumu Ngunyale alisema baada ya kupitia pande zote za mashidi tisa
walioletwa na upande wa mlalamikaji na mashihidi saba waliofikishwa mahakamani
hapo na upande wa mlalamikiwa , mahakama imeona hakuna ushahidi uliotosha
kuishawishi mahakama hiyo ili kuweza
kutengua matokea yauchaguzi huo.
“Baada yakupitia hoja zote mahakama imeona mlalamikaji hakuweza kuleta ushahidi
unaotosha kuishawishi mahakama itenguematokea hiya,hivyo mahakamainamtangaza
Joseph Ryata kuwa mshindi halali wa kiti hico cha udiwani”alisema Ngunyale.
Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo wakili aliyekuwa
akimwakilishi mlalamikia Alfred Mwakingwe alisema atakwenda kukutana na
mawakili wenzake pamoja na mteja wake ili wajadili na kuona hatua za kuchukua.
Naye wakili wa upande wa utetezi Baranabas Nyalusi alisema
mahakama imemtendea haki mteja wake na kushauri
wanasiasa kuwa na utaratibu wa kukubari matokea pindi wanapotangwa kuwa
wameshindwa uchaguzi na kujipanga kwauchaguzimwingine.
Hamid Mbata ambaye alishindw akatika kesi hiyo alisema
anasubiri apate hukumu iliyotolewa mahakamani hapo kwa maandishi na baada ya
kuipitiana kuitafakari ataamua cha kufanya.
Naye Ryata ambaye pia ni Naibu Meya wa Halmashauriya
Manispaa ya Iringa aliishukuru mahakama kwa kutenda haki na kuahidi kufanya
kazi zaidi ya ilivyokuwa mwanzo kwa kuwa alipoteza muda mwingi mahakamani alikokuwa anakwedna
kusikiliza kesi.
MWISHO
0 maoni:
Chapisha Maoni