Alhamisi, 25 Agosti 2016

MAHMOUD MGIMWA AKABIDHI MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE YA SEKONDARI YA MDABULO.

Postedy by Esta Malibiche on August 25.2016 in News with No comment



MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa akihutubia wananchi waliofika kwenye mkutano uliyafanyika kwenye shule ya sekondary Mdabulo.


 
Baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini mahamood mgimwa

 


Picha zote na Fredy Mgunda

 MBUNGE wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa amekabidhi mifuko 100 ya saruji na ndoo kumi za rangi zenye ujazo wa lita ishirini kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya ya kukarabati majengo ya shule ya sekondari ya Mdabulo iliyopo Kijiji cha Mdabulo wilayani mufindi.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo,Mgimwa alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano kuto kipaumbele katika Elimu ili kuweza kujenga jamii imara ni lazima kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira stahihiki
Mgimwa alisema lengo la kutoa msaada huo, ni kutokana na shule hiyo kuwa chakavu katika maeneo muhimu kama kwenye mabweni na bwalo ambalo hutumiwa na wanafunzi kwa ajili ya chakula.
“Baada ya kupata taarifa hizi, nimeamua kuja na mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi ili waangalie namna ya kufanya marekebisho katika madarasa pamoja na mabweni ya shule hii na nimewaagiza wahakikishe wanakarabati shule hiyo na iwe kwenye viwango vinavyotakiwa,” alisema Mgimwa.
Mgimwa aliwataka wanafunzi wasome kwa bidii ili waweze kufaulu na si kusoma ili kupata ajira kama ilivyozoeleka kwa watu wengi kwani serikali inafahamu changamoto ya ajira iliyopo.
 
  “Sina budi kuunga mkono juhudi zenu za ujenzi wa Shule ya sekondari ya Mdabulo, ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi, nami kama mwakilishi wetu ninaungana nanyi kwa dhati na katika hili napenda kukabidhi mifuko ya saruji.
 
Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema huku wakisaidiana na walimu kwa kushirikiana katika nyanja ya elimu ili kupanua wingo wa ufaulu kwa wanafunzi.
 
 Nimekuwa na ziara katika jimbo langu nikiwa na  lengo la kutimiza ahadi zangu nilizoahidi kipindi cha kampeni za chaguzi muu 2015.Kilichabaki hiki sasa ni kuwatekelezea wananchi ahadi nilizoahidi ili jimbo letu liweze kusonga mbele'''alisema Mgimwa 
 
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamuhuri Willium,akimshukuru mbunge huyo   kwa kuunga mkono juhudi za wananchi za kuinua sekta ya elimu katika jimbo lake.
Jamuhuri alisewasihi wazazi kuwahimiza watoto wao kujituma katika masomo na  kufuatilia maendeleo pamoja na  kuwapa muda wa kujisomea mara warudipo nyumbani.

'''Wazazi wengi wanashindwa kuwatengea muda wa kujisomea watoto wao,wanawarundikiakazi ngumu,halii hii inasanabisha kiwano cha ufauru kupungua.Ninawaomba tuzingatie Elimu kwa watoto wetu'''alisema Jamuhuri
 
 Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Geogrge Mgomba, alimshukuru mbunge kwa mchango wake huo,na aliwasihi  wanafunzi wake kusome kwa ajili ya ajira binafsi na si kutegemea ajira kutoka serikalini kwa kuwa serikali ina mzigo mkubwa.
 “Wanafunzi mnatakiwa msome kwa bidii na msitegemee ajira kutoka serikalini, mtafute ajira binafsi au kujiajiri wenyewe,”alisema

0 maoni:

Chapisha Maoni