Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwa anachangia hoja.
………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, UTETE RUFIJI
MBUNGE wa jimbo la Rufiji Mkoani Pwani Mohamed Mchengerwa
ameahidi kulivalia njuga suala la migogoro ya ardhi inayotokana na jamii
ya wafugaji na wakulima ambao wamekuwa wakigombania maeneo ya mashamba
na kusababisha kutokea kwa mapigano ambayo wakati mwingine yanapelekea
uvunjifu wa amani.
Kuwepo kwa hali hiyo ya migogoro ya ardhi kwa wakulima na
wafugaji katika halmashauri ya Rufiji kunatokana na baadhi ya wafugaji
kuamua kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa na kwenda kulisha
mifugo yao katika maeneo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya shughuli
mbali mbali za kilimo.
Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa wa viongozi katika
halmashauri hiyo mpya ya ya rufiji, ambapo alisema mesema hawezi
kuwavulilia wale wote ambao wataonekana wanakwenda kinyume cha sheria za
nchi, na kuhakikisha kila mfugaji na mkulima anatengewa maeneo yao
rasmi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao lengo ikiwani kuepukana na
migogoro na mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza kutokana na
kugombania ardhi.
Aliongeza kwamba nia yake kubwa ni kuhakikisha
naweka mikakati kabambe ambayo itaweza kuwawasaidia wananchi wake
wakiwemo wafugaji na wakulima kwa kushirikina na viongozi wa halmashauri
katika kuwatenge maeneo yao maalumu ambayo yataweza kusaidia kuepukana
na migogoro hiyo ya ardhi.
“Mimi kama mbunge wa jimbo hili la rufiji ninatambua kuwepo
kwa changamoto kubwa na mogogoro katika ya wakulima na wafigaji, laki I
dhamora yangu kubwa nataka nione wanachi wangu wa jimbo la rufiji
wanakaa kwa amani bila ya kuwepo kwa mapigano yoyote kwa hiyo ili
nitalivalia njuga na kuhakikisha kwamba sula la amani na utulivu
linakuwepo,”alisema Mchengerwa.
Aidha alisema kwamba anatambua wananchi wa jimbo lake
wanategemea sana shughuli za kilimo hivyo kwa sasa wameshaweka utaratibu
wa kutenga maeneo ya wafugaji ili wasiweze kuingia katika mashamba ya
wakulima na kupelekea vurugu z amara kwa mara kitu amabcho sio kizuri na
kinarudisha nyuma maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa halmashauri ya Wilaya ya
Rufiji Saidina Malenda mara baada ya kushindakatika uchaguzi huo
alisema atahakikisha nasharikina bega kwa began a viongozi wenzake kwa
lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wa
Rufiji.
Malenda aliongeza kuwa anawashukuru madiwani wenzake kwa
kuweza kumchagua kuwaongoza na kubainisha kwamba atafanya kazi bidii
zote na kwa kushirikina katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo bila ya
kuwa na ubaguzi wa aina yoyote wa itikadi ya vyama ili kuweza
kuwatumikia wananchi katika huduma mbali mbali wanazozihitaji.
Katika uchaguzi huo wa halmashauri mpya ya Wilaya ya
Rufiji,uliofanyika utete nafasi ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Saidani
Malenda ambaye alipata kura 11 kati ya kura 19 zilizopigwa, ambapo
nafasi ya Makamu mwenyekiti ilikwenda kwa Hawa Mtopa ambaye aliyepata
kura 10 katika ya kura 19 zilizopigwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni