Kufuatia
kuvunjika kwa mkutano mkuu maalum wa CUF uliokuwa na lengo la kuziba
nafasi ya mwenyekiti wa chama baada ya aliyekuwa mwenyekiti, Prof.
Ibrahim Lipumba kujizulu, chama hicho kupitia Mkueugenzi wa Habari,
Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Salim Biman kimetoa taarifa, waweza
isoma hapa.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA YA AWALI YA CHAMA CHA CUF JUU YA KILICHOTOKEA KATIKA MKUTANO MKUU MAALUM WA TAIFA ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA HOTEL YA BLUE PEARL –UBUNGO PLAZA, DAR ES SALAAM;
TAARIFA YA AWALI YA CHAMA CHA CUF JUU YA KILICHOTOKEA KATIKA MKUTANO MKUU MAALUM WA TAIFA ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA HOTEL YA BLUE PEARL –UBUNGO PLAZA, DAR ES SALAAM;
IMETOLEWA LEO TAREHE: 22/8/2016
Jana tarehe 21/8/2016 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano mkuu maalumu wa taifa katika ukumbi wa hotel ya blue pearl –ubungo plaza, dar es salaam.
Jana tarehe 21/8/2016 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano mkuu maalumu wa taifa katika ukumbi wa hotel ya blue pearl –ubungo plaza, dar es salaam.
Chama
cha cuf kinapenda kutoa taarifa rasmi za awali juu ya kilichotokea.
Baraza kuu la uongozi la taifa la chama cha cuf liliitisha mkutano mkuu
huo kwa madhumuni ya kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi wazi ikiwemo ya
mwenyekiti wa chama taifa kutokana na aliyekuwa mwenyekiti wa chama
taifa prof. Ibrahimu lipumba kujiuzulu katika nafasi hiyo tarehe
5/8/2016.
Mkutano
mkuu maalum wa taifa ulitimiza akidi ya wajumbe halali waliopaswa
kuhudhuria katika mkutano huo. Kwa mujibu wa katiba ya chama (1992)
ibara ya 79(3) toleo la mwaka 2014 wajumbe wa mkutano mkuu walimchagua
mheshimiwa julius mtatiro kuwa mwenyekiti wa kuongoza kikao hicho cha
mkutano mkuu kutokana na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chama taifa kuwa
wazi .
Wajumbe
wa mkutano mkuu walizikubali na kuzithibitisha ajenda mbili za mkutano
huo zilizoandaliwa na kuwasilishwa na baraza kuu la uongozi taifa ambazo
ni;
Ajenda ya kwanza kupokea taarifa ya barua ya kujiuzulu kwa prof. Ibrahim lipumba, na ajenda ya pili ni kujaza nafasi wazi ya mwenyekiti wa chama taifa, makamu mwenyekiti taifa na wajumbe wanne wa baraza kuu la uongozi taifa.
Ajenda ya kwanza kupokea taarifa ya barua ya kujiuzulu kwa prof. Ibrahim lipumba, na ajenda ya pili ni kujaza nafasi wazi ya mwenyekiti wa chama taifa, makamu mwenyekiti taifa na wajumbe wanne wa baraza kuu la uongozi taifa.
Baada
ya kuwasilishwa ajenda ya kwanza na wajumbe kupata nafasi za kuijadili
ajenda hiyo kwa uwazi na kina, huku kukiwa na mitazamo tofauti, ghafla
aliyekuwa mwenyekiti wa chama taifa prof. Ibrahimu lipumba alilazimisha
kwa nguvu kuingia ndani ya ukumbi akifuatana watu ambao si wajumbe wa
mkutano mkuu huo na kuanzisha vurugu ndani ya ukumbi wa mkutano.
Viongozi wa chama na mwenyekiti wa mkutano huo waliweza kuwatuliza
wajumbe na kuendelea na kikao.
Kuhusu hitimisho la mjadala wa ajenda ya kwanza juu ya taarifa ya barua ya kujiuzulu kwa Prof. Ibrahim Lipumba.
Kwa
mujibu wa katiba ya chama (1992) ibara ya 117 (2) baada ya mjadala
wajumbe walikubaliana kufanya maamuzi juu ya kukubali na au kukataa
kujiuzulu kwa prof. Ibrahimu lipumba. Wajumbe wa mkutano mkuu walipiga
kura na matokeo ni kuwa wajumbe walioafiki maamuzi ya kujiuzuru kwa
prof. Ibrahimu lipumba walikuwa wajumbe 476 na waliokataa kujiuzulu
kwake walikuwa wajumbe 14 na wajumbe wengine hawakupiga kura ya kukubali
au kukataa.
Baada
ya matokeo hayo kutangazwa na wajumbe kurejea katika ukumbi kuendelea
na ajenda ya pili, huku mheshimiwa prof. Ibrahimu lipumba wakati wote
akiwa ndani ya ukumbi akishuhudia maamuzi hayo ya wajumbe, wajumbe
wachache waliokuwa wakikataa kujiuzulu kwa prof ibrahimu lipumba
wakishirikiana na wale alioingia nao walianzisha vurugu za kutotaka
kuendelea kwa ajenda ya pili ya kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi
zilizowazi.
Kutokana
na hali hiyo ya kufanya vurugu ndani ya mkutano mkuu, viongozi wa chama
taifa walishauriana na kuona kuwa busara ni kuahirisha zoezi hilo la
kujaza nafasi, na mwenyekiti wa kikao cha mkutano mkuu maalumu wa taifa
mheshimiwa julius mtatiro alifunga mkutano huo mpaka hapo wajumbe
watakapoarifiwa tena.
Baraza
kuu la uongozi taifa lilifanya mchujo wa wagombea tisa waliojaza fomu
na kupitisha majina matatu ya wagombea wa nafasi hiyo ya mwenyekiti wa
chama taifa ambao ni mheshimiwa twaha taslima, riziki shaali mngwali na
juma mkumbi.
Kwa nafasi ya makamu mwenyekiti waliopitishwa kugombea ni mheshimiwa salim biman na mheshimiwa mussa haji kombo.
Msimamo wa chama juu ya kadhia
Chama
cha wananchi-cuf kinapenda kuwataarifu na kuwahakikishia wanachama,
wapenzi wa chama chetu na marafiki zetu wote kuwa cuf ni taasisi kubwa
ya kisiasa nchini iliyo na viongozi makini na mahiri. Tunawaomba wajumbe
wote wa mkutano mkuu wa taifa na wanachama wetu wote na watanzania kwa
ujumla kuwa watulivu katika kipindi hichi, na kuzipuuza taarifa zote
zenye lengo la kupotosha usahihi wa suala hili.
Mchakato
wa kukamilisha zoezi la kujaza nafasi wazi za uongozi wa chama taifa
upo palepale na baada ya kukamilisha taratibu za ndani ya chama tutatoa
taarifa kwenu na kwa watanzania wote.
Ni
muhimu kukumbukwa kwamba ajenda ya kwanza ya msingi katika mkutano mkuu
huu imekamilika kwa wajumbe wengi wa mkutano mkuu wa chama taifa
kukubali kujiuzulu kwa mheshimiwa prof. Ibrahimu lipumba.
HAKI SAWA KWA WOTE
SALIM BIMAN
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO KWA UMMA.
SALIM BIMAN
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO KWA UMMA.
0 maoni:
Chapisha Maoni