Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU)zimekosoa kitendo cha kuvunjika kwa mazungumzo kati ya viongozi na waasi wa Sudan kilichoteka wiki ya hivi karibuni kuhusu kusitisha uhasama na mzozo katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema amevunjwa moyo kufuatia kuvunjika mazungumzo ya pande zinazozozana huko Sudan kuhusu kufikia mapatano ya kusitisha uhasama huko Darfur, Blue Nile na Kordofan ya Kusini.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesisitiza kuwa, hakuna njia mbadala ya kudumu ya kuupatia ufumbuzi mzozo huo wa Sudan baada ya kughairishwa mazungumzo hayo.
Aidha mwakilishi wa Umoja w Afrika amewasilisha ujumbe tofauti na kulaani kuvunjika mazungumzo hayo kati ya makundi ya Sudan huko Addis Ababa na kusisitiza kuwa pande hizo zimepoteza fursa ya wazi ya kufikia mapatano ya kudumu.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa, hadi kufikia sasa zaidi ya watu laki tatu wamepoteza maisha huko Sudan na wengine zaidi ya milioni moja wamelazimika kuwa wakimbizi kufuatia mchafuko yaliyolikumba eneo la Darfur.
Na Regina Mkonde