Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akichangia jambo wakati wa kikao kazi cha Idara ya Mazingira kilichoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira na Wakuu wa Vitengo, waliokaa pamoja na Makamu wa Rais kushoto ni Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Mbaraka Abdulwakil.
...........................................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka
watendaji wa Idara ya Mazingira katika ofisi yake wajipange vizuri kwa ajili ya
kufanya tathmini ya athari za kimazingira mjini Dodoma wakati serikali
ikijiandaa kuhamia kwenye mji huo.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo 21-Aug-16
alipokuwa akifunga mkutano wa kazi wa siku mbili na watendaji wa Idara ya
Mazingira ambapo walijadili namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira
unaoendelea kote nchini.
Ameeleza
kuwa hatua hiyo itasaidia kuuweka mji wa Dodoma salama kimazingira ikiwemo
ubora wa miundombinu za maji taka.
Makamu
wa Rais amesema kutokana na idadi kubwa ya watu hasa watumishi ambao watahamia
Dodoma bila miundombinu imara hali ya uchafuzi wa mazingira itakuwa si nzuri
hivyo ni muhimu kwa watendaji hao kuweka mipango na mikakati madhubuti ya
kuhakikisha mji wa Dodoma hautaathirika kimazingira.
Kuhusu
utendaji kazi wa watumishi wa ofisi yake amewataka watumishi wote kufanya kazi
kwa ushirikiano na kwa uwazi katika matumizi ya fedha za miradi na hasa inayohusika na uhifadhi wa mazingira jambo
ambalo litaondoa manung'uniko miongoni mwa watumishi na wananchi kwa ujumla.
Amesema
ushirikiano huo miongoni mwa watumishi utasaidia kwa kiasi kikubwa ufanisi
katika kazi za kila siku ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Makamu
wa Rais amesema ataendelea na utaratibu wa kukutana na watumishi kila baada ya
miezi 4 katika ngazi ya viongozi kama hatua ya kujitathmini katika mipango
ya kazi waliyojiwekea.
0 maoni:
Chapisha Maoni