Postedy by Esta Malibiche on August 22.2016 in News with No Comment
Na Esta Malibiche
Iringa
KATIBU tawala wa Wilaya ya Iringa Joseph chitinka amewasihi
Vijana kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujiajili wenyewe ili waweze kuondokana na dhana ya kuisubiri
serikali iwaajiri
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akifungua semina ya mafunzo ya
ujasiliamali kutoka shirika la Right way for development [Riwade]ambalo
linafanya kazi ya kuwasaidia vijana wasio na ajira kufanya kilimo,ufugaji,uvuvi
kuwa ni moja ya ajira.Mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani hapa na kuhudhuriwa navijana kutoka wilaya Kilolo,Mufindi,Iringa vijijini,Manispaa ya Iringa na
Halmashauri ya mji wa Mafinga.
Mafunzo hayo yaliwahusisha vijana ambao bado hawajapata ajira
bado baada ya kuhitimu vyuo mbalimbali,wakulima na wafugaji na wajasiliamali.
Chitinka alisema kuwa serikali pekee haiwezi kutoa ajira kwa
vijana wote wanaohitimu vyuo nchini,bali
vijana wanatakiwa kujiajili wenyewe kwa
kuchangamkia fursa zilizopo hasa katika kilimo ili waweze kujikwamua
kimaishana kujipatia maendeleo.Pia alisema
ili mjasiliamali aweze kupiga hatua anatakiwa ajitambue mwenyewe pamoja na kutambua mazingira
yanayomzunguka.
‘’’’’ Mkoa wa Iringa una utajili wa ardhi yenye rutuba
,endapo vijana watachana na tabia ya kukaa vijiweni asubuhi na kucheza michezo
isiyo na manufaa kwao na kuamua kufanya
kazi kwa bidii katika kilimo wataweza kujikomboa na wimbi la umasikini ‘’’’alisema
Chitinka
Tunapata matumaini makubwa na Serikali iliyopo madarakani
kutokana na kuhimiza kila mmoja wetu afanye kazi kwa juhudi.Tuwekeze kwenye
vitu vya msingi ambavyo vinaweza kutuletea maendeleo endapotukipata mikopo
kutoka Riwade.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Riwade Ayubu Masau akiendesha
semina kwa vijana wahitimu vuyuo vikuu wasio na ajira alisema kuwa vijana waliowengi wamejitengenezea dhana ya
kuwa mara wamalizapo vyuo wanasubiri serikali iwaajiri na si kujiari.
Ile dhana ya kuajiliwa inatakiwa iondolewe miongoni mwa
vijana na hatimae waweze kujiajili kwa kutumia fulsa zilizopo na zinazotolewa
na serikali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali’’’’’
Alisema tatizo kubwa la ajira kwa vijana linatokana na
Elimu tunayoipata,hivyo kwa kupitia shirika la Riwade vijana wanatakiwa
kusimama kwa kujiajili bila kusubiri kuajiliwa na serikali pekee
Masau alisema kupitia sekta ya kilimo,uvuvi na ufugaji inaweza
kupunguza changamoto kubwa ya ajira kwa
vijana nchini endapo vijana watajitambua na kukaa pamoja kwa kupanga mikakati
yao mara wamalizapo vyuo.
‘’’’’’Lengo la Riwade ni kuwasaidia vijana wasio na ajira
waweze kufanya kilimo,ufugaji,uvuvi wa kisasa ulioendelevu na mazingira kuwa ni
ajira tosha inayoweza kumkomboa kijana.Pia inawahusisha wakulima katika ngazi
zote ili kuweza kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya
kilimo,uvuvi, ufugaji na mazingira kwa
ujumla.
Alisema kuwa dira ya Riwade ni kuziboresha huduma za jamii
ambazo zinapelekea ukuaji wa hali ya kiaisha kwa wananchi.Pia inatengeneza na
kutoa fursa kwa watanzania wote ili waweze kupata Elimu ya ujasiliamali na
namna ya kutengeneza mitaji ya ukuaji endelevu wa kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo,Josiah Kifunge ni
muhitimu wa chuo kikuu Iringa [Tumaini] toka mwaka 2012 hadi sasa hajapata
ajira serikalini na, ameamua kujishugulisha na ujasiliamali katika kilimo, alilishukuru
shirika la Riwade na kusema kuwa mafunzo waliyoyapata watayatendea kazi
ipasavyo.
‘’’’’Mimi binafsi baada ya kuhitimu chuo nilikuwa na wazo la
kuajiliwa lakini nimeakaa zaidi ya miaka mine sijapata ajira,nimeamua kujiajiri
kwa kujikita katika kilimo.Zaidi nalima mazao ya mbogamboga na nimeweza kupiga hatua ‘’’’
Nimefundisha semina
nyingi na nimehudhuria semina nyingi za ujasiliamali,hii ya leo imeweza kugusa
mahitaji ya vijana wahitimu wasio na ajira na kuwawezesha kujiajiri pasipo
kusubiria kuajiliwa.Riwade wamejibu changamoto za vijana waliowengi wasio na
kipato.
Kifunge aliongeza kuwa
semina nyingi za ujasiliamali
wakufunzi huwa wanatoa mafunzo na kuwaacha washiriki wake njia panda
bila ya kuwapa mwongozo na namna ya kujikwamua,lakini semina iliyotolewa na
Riwade imeweza kuwaunganisha kwa pamoja.
Mkurugenzi wa shirika la RIWADE Eng.Ayubu Masau akitoa semina elekezi kwa vijana [hawapo pichanai]kuhusu kujialiri |
Semina ikiendelea huku washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizoendeshwa na mkurugenzi wa RIWADE,Eng.Ayubu Massau
Mkurugenzi wa RIWADE Eng.Ayubu karikati mwenye shati la kitenge akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa semina kutoka Manispaa ya Iringa |
Mkurugenzi wa RIWADE Eng.Ayubu karikati mwenye shati la kitenge akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa semina kutoka wilaya ya kilolo |
Mkurugenzi wa RIWADE Eng.Ayubu karikati mwenye shati la kitenge akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa semina kutoka Wilaya ya Mufindi |
Mkurugenzi wa RIWADE Eng.Ayubu karikati mwenye shati la kitenge akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa semina kutoka Halmashauri ya Mji wa Mafinga |
Mratibu wa RIWADE Mkoa wa Iringa Vumilia,akiwa na mshiriki wa semina Josiah Kifunge, muhitimu katika chuo kikuu Iringa[Tumaini]ambae ni mjasiliamali wa kilimo cha mbogamboga. |
Baadhi ya washiriki kutoka kila wilaya zilizopo mkoani
Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa RIWADE Tanzania
Eng.Ayubu Masau Picha zote na Esta Malibiche[KALI YA HABARI BLOG] |
0 maoni:
Chapisha Maoni