Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wataalam wa
Tehama wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu hao
uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Prof.
Faustine Kamuzora akiongea na wataalam wa Tehama wakati wa uzinduzi wa
mkutano wa siku moja wa wataalamu hao uliofanyika jijini Dar es Salaam
leo.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wanahabari
hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mkutano wa siku moja wa wataalamu
hao uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Benjamin Sawe)
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kikao hicho.
………………………………………………………………………
Na Abushehe Nondo,MAELEZO.
Naibu Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ameiagiza Tume ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano nchini kuhakikisha wanatengeneza misingi ya
uadilifu wa kitaaluma na misingi hiyo itumike kuwadhibiti wale ambao
wanatumia utaalamu huo kwa nia ovu.
Mhandisi Ngonyani aliyasema hayo
wakati akizindua mkutano wa kwanza ambao umeandaliwa ma Tume mpya ya
Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) uliofanyika katika ukumbi wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alisema Mkutano huo una lengo la
kuwakutanisha wataalamu wa TEHAMA kutoka katika sekta za umma na sekta
binafsi ili kuweza kujadiliana ni kwa namna gani taaluma hiyo inavyoweza
kutumika zaidi kwa faida ya ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
“Wapo baadhi ya watu wanatumia
taaluma ya TEHAMA kwa manufaa mbalimbali ya kujenga uchumi na maendeleo,
lakini wapo wachache ambao wanatumia utaalamu wao kwa manufaa binafsi
ikiwemo kuwadhalilisha watu wengine na kuwaibia fedha zao katika
mitandao” Alisema Mhandisi Ngonyani.
Alisema Tume hiyo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano inatakiwa kuja na sheria kali ambazo zitawabana
wale wote ambao wamekua na tabia ya kutumia mitandao katika kufanya
vitendo viovu badala ya kutumia katika kujiletea maendeleo.
Awali akizungumza katika mkutano
huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano upande
wa sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora alisema uanzishwaji wa
Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini ni jitihada za
makusudi za serikali katika kukuza Mawasiliano .
Prof,Kamuzora alisema kuwa tume
hiyo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa na hivyo kuwasihi
watendaji hao kuwaelimisha zaidi wananchi kujikita zaidi katika kufuata
maadili ya taaluma hiyo ili kulifikisha Taifa katika mafanikio ya sekta
ya mawasiliano.
Alisema Tume ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano itasaidia kukuza uchumi wa Taifa kutokana na kukua
kwa sekta ya TEHAMA na kuchochea uzalishaji ,ukuaji wa sekta zingine
kiuchumi na usambazaji wa huduma za jamii.
0 maoni:
Chapisha Maoni