Postedy by Esta Malibiche on August 26.2016
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
akizungumza na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Misaada la
Japan,(JICA) Bw. Hiruchi Kato (kulia kwake) na ujumbe wake , jijini
Nairobi Agosti 26, 2016 ambako anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa sita
Wa Tokyo International Conference on Africa Development (TICAD). Kushoto
kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Japan Mathias Chikawe. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………..
*Kampuni Chiyoda kufundisha Watanzania masuala ya gesi
*JICA kusaidia ujenzi wa miundombinu Dodoma
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewasili Nairobi, Kenya kuhudhuria Mkutano wa Mkuu wa Sita wa Wakuu wa
Nchi wa TICAD (TICAD VI) utakaofanyika Agosti 27 -28, mwaka huu. Waziri
Mkuu anahudhudia mkutano huo kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Leo asubuhi (Ijumaa, Agosti 26,
2016) Waziri Mkuu amekutana na viongozi wakuu mbalimbali wa makampuni ya
kibiashara kutoka Japan ambao wamekuja kuhudhuria mkutano huo.
Waziri Mkuu amekutana na Makamu wa
Rais wa Kampuni ya Chiyoda Corporation, Bw. Tadashi Izawa ambapo katika
mazungumzo yao, pamoja na kuangalia fursa nyingine katika sekta ya gesi
Tanzania, kampuni hiyo imekubali kutoa mafunzo ya kujenga uwezo wa
wataalamu kwa sekta ya gesi hususan usindikaji wa gesi kwa ajili ya
kusafirisha nje ya nchi (Liquefied Natural Gas).
Bw. Izawa amemweleza Waziri Mkuu
kwamba wamefurahiswa na taarifa za ugunduzi wa gesi ya Helium hapa
nchini Tanzania na kwamba kampuni yake ina teknolojia na uzoefu wa muda
mrefu katika kutekeleza miradi ya gesi (Gas value Chain Planning and Execution).
“Tunao uzoefu wa muda mrefu, pia
tunazo teknolojia za kuendeleza sekta ya gesi ikiwemo Helium kwa mfano
ujuzi wa kutenganisha gesi asilia na helium (Separation of Natural Gas
and Helium). Tumetekeleza miradi ya namna hii nchini Qatar ambayo kwa
sasa ni ya pili kwa uzalishaji wa gesi hiyo duniani ikitanguliwa na
Marekani,” amesema.
Amesema mafunzo hayo yatafanyika
kuanzia mwakani na yatalenga vijana wasiopungua 10 kutoka Tanzania ambao
wamehitimu shahada za uhandisi kwani wameshafanya hivyo kwa vijana
wanane kutoka Msumbiji.
Waziri Mkuu alimshukuru Vw. Izawa
kwa mpango wao wa mafunzo kwa vijana wa Kitanzania lakini akamtaka pia
waangalie uwezekano wa kuwasaidia vijana wanaotoka maeneo husika yenye
gesi ili wapatiwe mafunzo ambayo yatawawezesha kumudu baadhi ya kazi
kwenye viwanda vya kusindika gesi.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu
amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Misaada
ya Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato na kujadiliana mambo
kadhaa yakiwemo ya nishati na miundombinu.
Katika mazungumzo hayo, Bw. Kato
alimweleza Waziri Mkuu nia ya shirika hilo kuendelea kusaidia miradi
mbalimbali ya kilimo hapa nchini na hasa katika sekta za afya, maji,
kilimo na miundombinu ambazo imekuwa ikijihusisha nazo kwa muda mrefu
sasa.
Waziri Mkuu alimshukuru kwa
ushiriki wa shirika hilo kwenye miradi ya nishati ya Kinyerezi na
akamtaka aendelee kuisaidia Serikali ya Tanzania inainginia kwenye awamu
ya tatu ya Kinyerezi (Kinyerezi III).
Katika hatua nyingine, Balozi wa
Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe alimwoba makamu wa Rais hyo
waangalie uwezekano wa kuwekeza kwenye sekta za nishati na miundombinu
ya mkoa Dodoma hasa katika kipindi ambacho Serkali imeamua kuhamia huko.
“Tunaomba muangalie sana suala la
kuendeleza nishati ya umeme kwani nchi yetu imeamua kuwa nchi ya
viwanda. Tutahitaji kuwa na umeme wa kutosha kuendesha viwanda vya
usindikaji bidhaa zetu, lakini pia si mbaya mkiangalia suala la
kuboresha miundombinu ya barabara na usafirishaji katika mji wa Dodoma,”
amesema.
0 maoni:
Chapisha Maoni