Posyedy by Esta Malibiche on August 17.2016 in KITAIFA nO comment
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al Najem wakiwa wamekalia madawati mawili
kati ya 50 yaliyotolewa na Kuwait na kukabidhiwa kwake na balozi huyo
jijini Dar es salaam Agosti 17, 2016.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amepokea msaada wa sh. milioni 12 kutoka mashirika ya misaada ya Kuwait
kwa ajili ya kununulia madawati ili kupunguza tatizo hilo nchini. Pia
amepokea madawati 100 kutoka ubalozi wa Kuwait na taasisi ya Direct Aid ya nchi hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huo leo (Jumatano, Agosti 17, 2016), Balozi wa Kuwait nchini
Tanzania, Bw. Jasem Al Najem amesema msaada huo ni michango kutoka
mashirika ya misaada ya nchi yake ambayo yanatoa huduma mbalimbali hapa
nchini.
“Tumejipanga kukamilisha ahadi ya
madawati 600, tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wa Kuwait Fund, na
mashirika mengine. Kwa sasa tunachangia madawati, baadaye tutakwenda
kwenye ujenzi wa madarasa, hata ikibidi tutaenda kwenye ujenzi wa
shule,” alisema.
Balozi Najem amesema wanatoa
misaada hiyo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Magufuli za
kutaka wanafunzi wote wakae kwenye madawati.
Akitoa shukrani mara baada ya
kupokea msaada huo, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi wa Kuwait kwa moyo
wao wa kujitolea ikizingatia kuwa ni wiki tatu tu zilizopita
alikwishatoa msaada mwingine wa madawati kwenye shule ya msingi Chamazi,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Aliyashukuru pia mashirika ya
misaada kupitia Ubalozi huo, ambao wametoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa
madawati. Ametoa wito kwa mabalozi wengine, sekta binafsi na wadau wa
maendeleo watoe michango zaidi ili yapatikane madawati ya kutosha.
Mashirika yaliyotoa michango hiyo
ni African Relief Organisation (hundi ya sh. milioni 6), Al Furqaan
Islamic Centre (hundi ya sh. milioni 6), Taasisi ya Direct Aid (madawati
50 ya shule za Msingi) na ubalozi wa Kuwait (madawati 50 ya shule za
sekondari).
0 maoni:
Chapisha Maoni