Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijianda na mkutano wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu katika ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Hii ndio muonekano wa Ukumbi wa Mkutano wa Mandvulo Grand uliopo Lozitha mjini Mbabane Swaziland ambapo mkutano wa 36 SADC unafanyika.
Mkutano
wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC Troika Summit) unaowahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika umefanyika mchana huu katika
ukumbi wa Grand- Lozitha mjini Mbababe Swaziland.
Mkutano
huo wa Troika unaohusisha nchi Tatu ambazo ni za Utatu ikiwemo
Tanzania, Msumbiji na Afrika Kusini ambapo kwa kuzingatia utaratibu huo
mkutano huo unahudhuriwa
na Wakuu wa nchi na serikali wa Msumbiji kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo (SADC Organ Troika Summit) na Afrika Kusini kama mwenyekiti aliyetoka na Tanzania inatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Asasi hiyo.
na Wakuu wa nchi na serikali wa Msumbiji kama Mwenyekiti wa Asasi hiyo (SADC Organ Troika Summit) na Afrika Kusini kama mwenyekiti aliyetoka na Tanzania inatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Asasi hiyo.
Baadhi ya ajenda ambazo viongozi hao watajadili kwenye mkutano huo ni hali ya ulinzi na
usalama katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagascar na Lesotho, masuala ya upatanishi na utatuzi wa migogoro pamoja na maombi ya Burundi na Comoro kutaka kujiunga katika Jumuiya ya Mandeleo Kusini mwa Afrika- SADC.

Katika
mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Ufunguzi rasmi wa mkutano wa SADC utafanyika terehe 30-Aug-16 katika ukumbi wa Grand-Lozitha mjini Mbababe Swaziland ambapo pamoja na Mambo mengine mkutano huo utatoa zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika uandishi wa insha katika jumuiya hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni