Postedy by Esta Malibiche on August 19.2016
Chama
cha Wanahabari Wanawake nchini, TAMWA, kimewakutanisha wanahabari
kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, kujadili namna mafunzo yaliyotolewa na
chama hicho kwa wanahabari hao wakati wa kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu
wa mwaka jana, kwa kuangazia usawa wa kijinsia kati ya Wanawake na
Wanaume katika mchakato wa uchaguzi huo.
Pichani
ni wanahabari hao wakiwa kwenye semina ya siku mbili kuanzia leo,
inayofafanyika Jijini Mwanza, ambapo imelenga kujadili namna mafunzo
yaliyotolewa mwaka jana na TAMWA kwa kushirikiana na taasisi ya
INTERNEWS yalivyosaidia katika suala la usawa wa kijinsia kabla na baada
ya uchaguzi mkuu pamoja na changamoto zilizojitokeza.
Na George Binagi-GB Pazzo
Mkufunzi wa semina hiyo, Deodetus Balile, ambaye pia ni Mhariri gazeti la Jamuhuri.
Semina kwa Wanahabari Kanda ya Ziwa
Godfrida Jola (kulia) akiteta jambo na Edson Sosten (kushoto), wote ni Maafisa Miradi TAMWA.
Baadhi ya Wanahabari Kanda ya Ziwa, wanaoshiriki Semina ya TAMWA Jijini Mwanza
0 maoni:
Chapisha Maoni