Mbunge Risala akivishwa kitenge na walimu mara baada ya kuwasili katika viwanja vya shule ya sekondari Enaboishu iliypo Arumeru Arusha |
Vikundi mbalimbali vya sanaa vikiendelea kutumbuiza |
Mbunge wa viti maalum chadema Risala Kabongo amekusanya
kiasi cha Mill.18.2 katika harambee ya yakuchangia maendeleo katika ya Shule ya sekondari Enaboishu Arumeru iliyoko mkoani Arusha tarehe 27.8.2016.
Harambee hiyo iliambatana na sherehe ya kuadhimisha miaka 50
ya shule hiyo toka kuanzishwa kwake,pamoja na mahafari ya 48 ya kidato cha nne.
Mbunge Kabongo na familia yake walichangia kiasi cha Tsh.5
mill.na alifanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh.13.2,hivyo kufikia jumla ya kiasi
cha Ts.18.2 mill.
Aliwashukuru wananchi na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo kwa kumuunga mkono katika harambee hiyo aliyoiongoza akiwa mgeni rasm.
Alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya bweni la wasichana,vyoo vya kisasa,bwalo la chakula na maktaba ya kisasa,ambapo kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kitasaidia kutekeleza mahitaji hayo.
Alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya bweni la wasichana,vyoo vya kisasa,bwalo la chakula na maktaba ya kisasa,ambapo kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kitasaidia kutekeleza mahitaji hayo.
Pia aliwasihi wanafunzi kuzingatia masomo,kusoma kwa bidii ili waweze kukamilisha ndoto,na kuwataka kujiepusha na viashiria vinavyoweza kukatisha masomo yao na kuharibu ndoto zao za baadae.
0 maoni:
Chapisha Maoni