Na Mahmoud Ahmad Arusha
Katibu wa Uvccm mkoa wa Arusha
Ezekiel Mollel amesema kuwa umoja huo utaendelea na kuingia mikataba
mipya na wapangaji wake waliondani ya vibanda na si vingine.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati
akiongea na wanahabari ofisini kwake ambapo alikumbushia siku 14
walizotoa kwa wapangaji hao wa umoja huo wa vijana kuwa zimeisha na
yeyote atakaekadi hatua zitachuliwa.
Mollel alisema kimsingi
wamekubaliana kuingia mkataba mipya na wapangaji wote kwenye vibanda 49
vinavyomilikiwa na umoja huo kwa wapangaji kuingia mkataba wa mwaka
mmoja mmoja.
Akatanabaisha kuwa na wale
wapangaji waliowapangishia hapo mwanzo nao kuwapangishia waliomo wao
hawatawatambua na kuanzia mwezi ujao wataanza zoezi la kuingia mikataba
mipya.
Aliwataka wapangaji hao kufuata
maelekezo waliokubaliana kwenye kikao chao na wale walipangishia wengine
watakuwa wamejiondoa wenyewe huku aliendani ndie wataingia nae mkataba
mpya.
“Hiki kibanda no 46
tumekubaliana na mpangaji aliekuwepo ambaye tulimfungia kuendelea na
biashara na huyo na mmliki wa awali sisi hatumtambui kwa teyari
ameshajilipa mwenyewe”alisema Mollel.
Aidha akizungumzi eneo la
Barcelona lenye eka mbili ambalo pia linamilikiwa na umoja huo alisema
kuwa wametangaza zabuni za upangaji wa eneo hilo na atakayeshinda zabuni
ndio ataendesha eneo hilo.
Nae mwenyekiti wa umoja huo
mkoani hapa Lengai ole Sabaya alisema kuwa suala la nyumba za umoja huo
ambayo katibu aliekuwepo huko nyuma Kizigo alijiuzia kwa kiasi cha 3
milion kwenye eneo la Ngarenaro ataalipeleka ngazi za juu kwa maamuzi
zaidi.
Wiki mbili zilizopita Uvccm
mkoani hapa walitoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari ambapo
alikemea vikali mikataba iliyoingia ya upangishaji wa vibanda vya umoja
huo na kujikuta wakiwa hawana kitu huku fedha zikichuliwa na wapangaji
wao kwa mikataba minono ya 450,000 huku umoja huo ukiambulia 5000 kwa
kibanda namba 46 haliiliyopekea kuingia na sera mpya ya mikataba ya
vibanda hivyo
0 maoni:
Chapisha Maoni