Jumamosi, 20 Agosti 2016

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATENDAJI WA IDARA YA MAZINGIRA

4
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira, kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na kulia ni Katibu Mkuu Oisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbaraka Abduwakil Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi Idra ya Mazingira Bi. Esther Makwaia akiwasilisha taarifa ya hali ya Mazingira nchini kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu, Ikulu jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano na Watendaji wa Ofisi yake Idara ya Mazingira mara baada ya kupata taarifa za maendeleo, mipango na mikakati ya Idara hiyo, kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwenye mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Watendaji wa Idara ya Mazingira (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
                                                             ………………………………………….
Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0cm 5.4pt 0cm 5.4pt;
mso-para-margin-top:0cm;
mso-para-margin-right:0cm;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0cm;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-ansi-language:EN-US;
mso-fareast-language:EN-US;}

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  amekutana na kufanya mkutano wa kazi na watendaji wa ofisi yake ya Idara ya Mazingira kujadili kwa kina namna ya kukabiliana na hali tete ya uharibifu wa mazingira unaoendelea nchini.
Katika mkutano huo uliofanyika leo, Ikulu, Dar es salaam ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, Makamu wa Rais ameawaagiza watendaji wa idara hiyo waache kukaa ofisini na badala yake waende kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na
uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.
 
Alisema hali ya uharibifu wa mazingira ikiachwa iendelee kama ilivyo inaweza ikasababisha madhara makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwamo wataalam wa mazingira na wadau wa maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema baadhi ya watendaji wamekuwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira na kuonya wataobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali ili kukomesha tabia hiyo.
Baadhi ya watendaji waliotoa taarifa kuhusu hali ya mazingira nchini wamekiri kuwa hali ya uharibifu wa mazingira siyo nzuri hasa kwenye mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Manyara, Geita, Singida na Kilimanjaro.
 
Inakadiriwa kuwa takribani hekta 400,000 za misitu zinaharibiwa kila mwaka hali ambayo inapelekea baadhi ya wanyama kutoweka.
Watendaji hao wameiomba serikali iongeze bajeti ya kutosha ili waweze kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi.
Makamu wa Rais ametumia siku ya mapumziko ili kujadiliana na kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini. Mkutano huo wa kazi unaendelea tena hapo kesho.
 

0 maoni:

Chapisha Maoni