Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. |
Na Dotto Mwaibale
VIONGOZI wa Good News for All Ministry wameandaa mkutano mkubwa wa kitaifa wa maombi ya kumuombea Rais Dk. John Magufuli na Taifa kwa ujumba maombi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 25 Chato mkoani Geita.
Katika hatua nyingine viongozi hao wamesema wanaunga mkono azma ya Rais Magufuli ya kuhamishia serikali
Dodoma kwani ni jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu,
hivyo wameandaa mpango wa kumuombea kwa siku 1001 sawa na miaka mitatu ili afanikiwe.

Wakizungumza Dar es Salaam leo asubuhi viongozi hao kutoka Good News
for All Ministry walisema uamuzi wakuanzisha mchakato wa kuhamisha serikalini jambo la
kijasiri na unapaswa kuungwa mkono na watanzania wote kwani ni maono ya Baba wa taifa
Julius Nyerere.
Askofu Dk. Charles Gadi alisema tangu Baba wataifa kutangaza azma hiyo serikali zilizotangulia zimefanya jitihada mbalimbali za kuimarisha mji wa
Dodoma ili uweze kutumika kama mji mkuu na sasa umefika wakati muhafaka.
“Sisi kama viongozi wa dini tupo nyuma yake na tunaongeza nguvu zetu natunatoa wito kwa watu wotewaserikali kuhamia
Dodoma, kwani jambo hili litaharakisha maendeleo katika mikoa ya pembezoni,” alisema.
AidhaAskofu huyo alishangazwa na uvumi kuwa endepo baadhi ya watendaji waserikali wakihamia
Dodoma kutakwepo na migogoro katika ndoa nyingi kutokana na kutengana kwa baadhi ya familia.
Alisema ni vyema watu wakaheshimu maadili na kuishika misingi,
kwani kusafiri hakukufanyi ‘ukachepuka’.
“Hata ukiwa hapa Dar es Salaam unaweza kuchepuka tu,silazimaiwe
Dodoma, mambo yaliyowazi ni yetu ila ya liyofichwa ni ya Mungu,” alisema.
Mchungaji Leons Kajuna alisema RaisMagufuli hastishike na kelele za watu zinazobeza azma yake kwani kawaida ya watu kupinga jambo linaloanzishwa kabla hawajaona mafanikio yake.
“Si wakati tena wakukaa na kunung’unika kuna vitu serikali ikishaamua ni kuvipokea kwa shukurani,
kwani kufanya hivyo niishara ya nidhamu,” alisema.
kwani kufanya hivyo niishara ya nidhamu,” alisema.
Askofu Dk. Charles Gadi alisema mpango waliyo uanzisha wakumuombea Rais kwa siku
1001 utaanzia katika mkoa wa Geita wilayaniChato na unatarajiwa kuhudhuriwa na mkuu wa mkoa huo.
0 maoni:
Chapisha Maoni