Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Balozi wa
Israel nchini Tanzania anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za
Kenya na Uganda Mhe. Yahel Vilan (kulia) Ofisini kwake leo jijini Dar es
salaam. Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili kuhusu
uanzishwaji wa ushirikiano katika maeneo mbalimbali yatayoinufaisha
Tanzania na Israel kwenye sekta ya Afya.
Balozi wa Israel nchini Tanzania
anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za Kenya na Uganda Mhe. Yahel
Vilan (kulia)akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu mara baada ya kumtembelea
Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (katikati) akifurahia
jambo mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yake na Balozi wa
Israel nchini Tanzania anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za Kenya
na Uganda Mhe. Yahel Vilan (kulia) Ofisini kwake leo jijini Dar es
salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Wizara hiyo,
Agnes Kimemo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiagana na Balozi wa
Israel nchini Tanzania anayezihudumia pia nchi Afrika Mashariki za Kenya
na Uganda Mhe. Yahel Vilan (kulia) mara baada ya mazungumzo Ofisini
kwake leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………
* Wakubaliana Kuongeza Ushirikiano katika Mafunzo ya Wataalam wa Sekta ya Afya nchini
*Israel kuendelea kusaidia upasuaji wa watoto wenye ugonjwa wa Moyo kupitia Taasisi ya Save the Heart Institute* Israel kusaidia Ujenzi wa Chumba cha Wagonjwa Mahututi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa UDOM
Na. Mwandishi –Wetu -Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini Tanzania Mhe. Yahel Vilan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamekubaliana kuanzisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali ambayo yatazinufaisha Tanzania na Israel katika sekta ya Afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Israel nchini Tanzania Mhe. Yahel Vilan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamekubaliana kuanzisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali ambayo yatazinufaisha Tanzania na Israel katika sekta ya Afya.
Balozi huyo anayezihudumia nchi za
Afrika mashariki Tanzania, Kenya na Uganda katika mazungumzo na Waziri
wa Afya wa Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu ameyataja baadhi ya mambo ambayo
Israel imekua ikishirikiana na Tanzania kuwa ni pamoja na kudhamini
matibabu ya moyo kwa Watoto kupitia Taasisi ya Save Child Heart ya
Israel na Mafunzo ya madaktari bingwa na Wauguzi kutoka Hospitali
mbalimbali nchini.
“Tumekuwa na utaratibu wa kuleta
madaktari ili waje watoe huduma kwa wagonjwa pamoja na ujuzi kwa
wataalam wa Tanzania” Ameeleza Balozi Vilam na kuongeza kuwa
Israel imekuwa ikitoa mafunzo ya muda mfupi kwa wataalam kutoka Tanzania
hususani madaktari na Wauguzi.
Balozi huyo amesema kuwa Israel
imekua ikitoa mafunzo ya muda mfupi kwa wataalam hususani madaktari na
Wauguzi kutoka Tanzania na kuongeza kuwa wanao mpango wa kusaidia
uanzishwaji wa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika eneo ambalo
serikali ya Tanzania itapenda kuboresha huduma hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu ameishukuru
Serikali na Wananchi wa Israel kwa ushirikiano wanaouonyesha kwa
Tanzania katika eneo la tiba hususani kwenye udhamini wa matibabu ya
watoto wenye ugonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
kupitia madaktari bingwa wanaotoka katika nchi mbali mbali ikiwemo
Israel.
“Kupitia ushirikiano na Israel, Serikali tumeweza kuokoa
kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi
kwa matibabu, hadi sasa kati ya wagonjwa 400 waliokuwa wanasubiri
kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu nusu yao wamepatiwa matibabu
hapa nchini chini ya utaratibu huo”. Ameeleza Mhe Ummy.
Mhe. Ummy amemwomba Balozi wa
Israel kuongeza fursa zaidi za mafunzo ya fani ya Afya kwenye kada
nyingi zaidi ikiwemo kada ya wataalam wa maabara, wauguzi na madaktari.
Aidha, amemwomba Balozi wa Israel kuwezesha ujenzi wa chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa – Dodoma.
Amesema hatua hiyo inatokana na
uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma ambapo maboresho makubwa ya utoaji wa
huduma za afya yanatakiwa ili kuweza kuhudumia watu watakaohamia Dodoma.
Akikubali ombi hilo, Balozi wa
Israel Mhe. Yahel Vilan ameeleza kuwa wataalam kwa ajili ujenźi wa
chumba cha wagonjwa mahututi wanatarajia kufika nchini Tanzania mwezi
Septemba kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa ahadi ya balozi.
0 maoni:
Chapisha Maoni