Jumatatu, 29 Agosti 2016

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AKEMEA UTORO WA MADIWANI

Postedy by Esta Malibiche on August 29.2016 inSIASA

dc
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza na waandishi kukemea
hatua ya kuahirishwa Baraza la Madiwani leo kwasababu za kutotimia
akidi.


 
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro amekemea kitendo cha kuahirishwa kikao cha Baraza la Madiwani katika jiji la Arusha kuwa kinawanyima wananchi haki ya kuwakilishwa katika
baraza hilo linalojadili maendeleo.
Kikao hicho kimeshindwa kufanyika baada ya madiwani 14 pekee kuhudhuria katika ya madiwani 36 ambao ni wajumbe halali wa kikao hicho.
Meya wa Jiji hilo,Kalist Lazaro amesema amelazimika kuahirisha kikao hicho baada ya akidi kushindwa kutimia huku akidai baadhi ya madiwani wamejificha wakiogopa kukamatwa na polisi kwa kuhamasisha maandamano ya Septemba  Mosi.
Mkuu wa wilaya amepinga kauli hiyo ya Meya na kusema akiwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amewasiliana na Mkuu wa polisi wa wilaya(OCD)ambaye alikanusha taarifa za kutafutwa madiwani hao.
Aliwataka madiwani hao  watimize wajibu wao wa kuwawakilisha wananchi waliowachagua badala ya kutoa sababu zisizo na mashiko huku wakifahamu vikao vya baraza la madiwani vipo
kisheria na vina gharama kuviandaa.

0 maoni:

Chapisha Maoni