Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Clifford Tandari akifungua semina ya Wahariri
wa Vyombo vya habari kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo
hicho katika masuala mbalimbali ya uwekezaji na jinsi ambavyo kimekuwa
kikishughulikia na kurahisisha sekta ya uwekezaji na wawekezaji
kusajiliwa kwa haraka zaidi ili kuendelea na shughuli zao ikiwa ni
juhudi za kuhakikisha uwekezaji wa haraka na salama.
Juhudi hizi za TIC pia ni kuunga
mkono juhudi za Mh. Rais Dk John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa
nchi ya viwanda vidogo na vya kati na kuleta maendeleo na uchumi imara
kwa watanzania.
Kaimu Mkurugenzi huyo ameviomba
vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini kufanya kazi kwa karibu na
Kituo cha Uwekezaji cha TIC ili kuelimisha wananchi na wageni mbalimbali
wenye nia ya kuja kuwekeza hapa nchini. Semina hiyo imefanyika kwenye
ofisi za kituo hicho jijini Dar es salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Clifford Tandari akisisitiza jambo katika
semina hiyo wakati akifungua semina ya Wahariri wa vyombo vya habari
katika semina iliyofanyika kwenye ofisi za kituo hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Clifford Tandari akizungumza jambo na
wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kufungua semina hiyo.
Pendo Gondwe Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC akifafanua jambo wakati semina hiyoikiendelea.
Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. John Mnali akitoa mada kwa waandishi wa habari wakati semina hiyo ikiendelea.
Wakuu wa vitengo mbalimbali Kituo
cha Uwekezaji TIC Tanzania kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji na
Uwezeshaji Nakuala Senzia, Mkurugenzi wa Uwekezaji TIC Bw.John Mnali na
Mkurugenzi wa Utafiti na Mfumo wa Mawasiliano Bw. Ayubu Sizya.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizotolewa na watoa mada kutoka TIC.
Mkurugenzi wa Uwekezaji na
Uwezeshaji Nakuala Senzia akizungumza akitoa mada kuhusu uwekezaji na
taratibu zake wakati semina hiyo ikiendelea katika ofisi za Kituo cha
Uwekezaji Tanzania TIC leo.
Mkurugenzi wa Utafiti na Mfumo wa
Mawasiliano Bw. Ayubu Sizya akitoa mada katika semina hiyo, kulia ni
Mkurugenzi wa Uwekezaji na Uwezeshaji Nakuala Senzia na katikati ni Mkurugenzi wa Uwekezaji TIC Bw.John Mnali.
0 maoni:
Chapisha Maoni