Jumanne, 23 Agosti 2016

MAJAMBAZI WAUA ASKARI 4,WAZIRI MWIGULU ATOA TAMKO MAJAMBAZI KUSAKWA


 
 















''''Usiku huu nimefika Mbande - Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.'''''
'''Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri''''
''''Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu.'''''alisema Mwigulu

0 maoni:

Chapisha Maoni