Dk. Ummy ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
“Nafuta tozo ya kumuona daktari na matibabu kwa watoto wanaobakwa ili kuwasaidia wasio na uwezo kupata matibabu na kufanyiwa vipimo vitakavyowezesha upatikanaji wa ushahidi ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria, ” amesema.
Ameongeza kuwa “Narudia tena fedha ya kumuona daktari marufuku, sitakuwa na msamaha kwa mganga mkuu ambaye hospitali yake itawatoza fedha Mama mjamzito, mtoto wa chini ya miaka mitano na wazee.Muhimbili niiagize kuwa hakuna fedha za kumuona daktari na vipimo, lakini kwenye dawa nitaelewa kwa kuwa wanawajibu wa kuchangia, wananchi wanakatwa kodi ambazo hulipa madaktari mishahara na kununulia vifaa tiba. “
Dk. Ummy amesema anataka kuboresha usimamizi wa huduma za afya kwa waganga wakuu wa mikoa ili kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya.
“Bila ya kusimamia utekelezaji na uwajibikaji katika sekta ya afya huduma ya afya haitakuwa nzuri, ” amesema.
Na Regina Mkonde