Makamu
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA
mkoani Mwanza, Leopard Lema (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi hii leo
Jijini Mwanza kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara Afrika Mashariki
yanayotarajiwa kuanza Agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viwanja
vya Rock City Jijini Mwanza.
Wengine
ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (wa kwanza
kushoto), Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara
mkoani Mwanza (wa pili kulia) na Majid Igangula (wa kwanza kulia),
kutoka bodi ya Washauri TCCIA.
Makampuni
pamoja na wajasiriamali mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki
ikiwemo Tanzania, yametakiwa kutumia Maonesho ya Biashara ya Afrika
Mashariki katika kutangaza na kuuza bidhaa zao.
Makamu
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA
mkoani Mwanza, Leopard Lema, ametoa rai hiyo leo Jijini Mwanza, wakati
akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Maonesho hayo.
"Maonesho
haya yanatoa fursa kwa makampuni mbalimbali Afrika Mashariki
kujitangaza, kukutana na wateja wao, kutafuta wabia wapya wa kibiashara
pamoja na kufanya utafiti wa kimasoko". Ametanabaisha Lema.
Maonesho
hayo yanatarajiwa kuanza agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika
viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza na yanatarajiwa kushirikisha
wafanyabiashara kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na nje ya Afrika
Mashariki.
Makamu
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA
mkoani Mwanza, Leopard Lema (katikati), akiwa katika mkutano na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara
Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agost 26,2016 hadi Septemba
04,2016 katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.
Wengine
ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (kushoto),
Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani
Mwanza (kulia).
Wanahabari Jijini Mwanza, wakiwa katika
Mkutano wa TCCIA kuhusu Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki Jijini
Mwanza, uliofanyika leo.
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya
Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard
Lema, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari.
Taswira
ya Mkutano wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA,
na Wanahabari ulioketi hii leo Jijini Mwanza, kuhusu Maonesho ya
Biashara ya Afrika Mashari yanayotarajiwa kuanza Agost 26 mwaka huu
viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG
0 maoni:
Chapisha Maoni