Balozi wa Uganda nchini Tanzania
Bi. Dorothy Samali Hyuha akisaini kitabu cha maombolezo na kutoa salamu
za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekua Rais wa Pili wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Nigeria
nchini Bi. Abiola Sherif Deluya akitoa salamu za pole katika kitabu
maalumu kilichopo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli, Jijini
Dar es Salaam leo.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania
Bw. Jassem Al Najem ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea Ofisi ya
Makamu wa Rais leo na kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa
Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar.
Balozi wa Palestina nchini
Tanzania Bw. Hafen Shabit akisoma dua mara baada ya kutia saini kitabu
cha maombolezo kilichopo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli,
jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
0 maoni:
Chapisha Maoni