Postedy byEsta Malibiche onAugust 17.2016 in News
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko
(katikati), Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe
(kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
(TEC) Padre Ubadius Kidavuri wakiwa wameshikilia Kamusi hiyo mara baada
ya Uzinduzi 17 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko
(katikati) akiwa ameonyesha juu Kamusi ya Ukristo iliyoandikwa na Padre
Jordan Nyenyembe (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri 17 Agosti, 2016 Jijini
Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko
(katikati) akikata utepe kuzindua Kamusi ya Ukristo iliyoandikwa
na Padre Jordan Nyenyembe (kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Baraza la
Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri 17 Agosti, 2016
Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHSUM.
……………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga-WHUSM.
Serikali imempongeza Mwandishi
wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe pamoja na wadau wengine
waliohusika katika kufanikisha uandishi wa Kamusi hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa jana
Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko
ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Mhe. Waziri Nape Nnauye wakati wa Hafla
ya Uzinduzi wa Kamusi hiyo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Mhe.
Waziri Nape Nnauye, Bibi. Beleko amesema kwamba Padre Jordan Nyenyembe
anapongezwa kwa uandishi wa Kamusi hiyo kwani kunaonyesha juhudi za
kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili.
Alisema kwamba uandishi wa
Kamusi ni kazi ngumu na endapo maneno ndani ya Kamusi hayatafsiriwi sawa
sawa basi kuna uwezekano wa kusababisha chuki, ghasia na hata mapigano
na hasa maneno yanayohusiana na masuala ya imani ya dini Fulani.
“Ni matumaini yangu kwamba,
Kamusi hii itahamasisha na kurahisisha uelewa wa vitabu na maandiko
mbalimbali kwa usahihi na ufasaha kwa jamii na kuleta upendo, utulivu na
amani”, alisema Beleko.
Aliongeza kuwa Wamisionari wa
mwanzo wa imani ya kikristo walisaidia katika usahihishaji na uenezaji
wa lugha ya Kiswahili kupitia vitabu na nyaraka mbalimbali, aidha
walishiriki katika kuandika sarufi za Kiswahili, kamusi za kiswahili na
kutafsiri Biblia kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine hali ambayo
ilisaidia kukuza dini ya Ukristo na kukuza lugha ya Kiswahili.
“Lugha yetu ya Kiswahili kila
kukicha inazidi kukua na kupitia Kamusi hii tunaamini kwamba wasomaji
wataongeza maarifa na ufasaha na kudumisha umoja, amani na uzalendo”,
alisema Beleko.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri ambaye
aliliwakilisha Baraza hilo alieleza kwamba, ushirikiano kati ya
serikali na taasisi za kidhni ni jhambo mhimu katika kusukuma maendeleo
ya taifa.
“Katika Kanisa la Katoliki
Tanzania linaunga mmkono jitihada zote za Wasomi na Wataalam wote
wanaowezesha ujuzi na maarifa mbalimbali kidini na hata kielimu
kuwafikia Wananchi katika kukabiliana na changamoto, hivyo nachukua
nafasi kwa niaba ya Baraza, kumshukuru na kumpongeza Padre Jordan kwa
jitigada zake za kubuni na kufanya kazi hii njema kwa Watanzania”,
alisema Padre Ubadius.
Naye Mwandishi wa Kamusi hiyo,
Padre Jordan Nyenyembe alisema kwamba Kamusi hiyo inakamilisha kazi
iliyoanza mwaka 2004 kama Makala katika Gazeti la Kiongozi iliyoitwa ‘Kiswahili cha Mwanakanisa’.
Alisema kwamba, wasomaji
watakaokuwa wanaitumia Kamusi hiyo wawe huru kumshirikisha kwa kutoa
maoni yao mbalimbali ili aweze kuboresha katika matoleo yajayo.
“Mtakaoisoma Kamusi hii msisite kutoa maoni yenu ambayo yataniwezesha kuboresha katika matoleo yajayo”, alisema Padre Jordan.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni
ya Uchapishaji Vitabu ya Mkuki na Nyoka, Bw. Walter Bugoya alieleza
kwamba, kuandaa kamusi kama hiyo kunahitaji mtu kufahamu masuala mengi
ambayo anatarajia kuyaandika, hivyo anakuwa na kazi kubwa ambayo
inahitaji umakini, kutafuta maana sahihi ya maneno.
“Pia katikia suala la uhalili
Mwandishi anahitaji kusaidiwa na Wahariri ili kazi yake iwe rahisi kwa
wasomaji kwa kupata maana sahihi ya maneno ndani ya kitabu husika”,
alisema Bw. Bugoya.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi alisema
kuwa, suala la lugha kwenye Makanisa ni muhimu sana kwani litasaidia
kukuza uelewa wa mafundisho ya imani ya dini hiyo, hivyo amepongeza kazi
ya uandishi wa Kamusi hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni