Alhamisi, 25 Agosti 2016

WASANII WAPENDA AMANI WAUNGANA KUPINGA MAANDAMANO YA UKUTA.

ash1
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wasanii wapenda Amani nchini, Asha Baraka akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya tamko lao la kuungana pamoja kupinga Maandamano ya UKUTA, Septemba 1.  
ash2
Mwenyekiti wa Umoja huo, Steven Mengere (Steve Nyerere) akizungumza juu ya kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika  Septemba Mosi kote nchini.
…………………………………………………………..
WASANII mbalimbali wanaopenda amani wameungana kwa pamoja kupinga maandamano ya UKUTA yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi, mwaka huu.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Wasanii hao wapenda amani, Steve Nyerere amesema hamna haja ya maandamano bali tunahaja ya kufanya kazi hususan kwa vijana.
“Vijana ndio muhimili mkubwa kulinda amani ya nchi,tusiwaze maandamano bali tuwaze je Akinamama na Watoto wanapata huduma hospitali”alihoji Steve Nyerere
Kwa Upande wa Makamu Mwenyekiti wa Wasanii hao, Asha Baraka amesema wameamua kupaza sauti zao kwa niaba ya Wasanii wote wanaopenda amani
Amesema Tanzania ni nchi ya Amani sio nchi ya vita hivyo wanapofanya shughuli za UKUTA shughuli zote za kijamii zitasimama.
Hatahivyo ameomba Septemba 1,  UKUTA wasimamishe maandamano hayo, pia watafute njia muafaka ya kuweza kuongea Vyama kwa Vyama na wakapata muafaka ili nchi iweze kwenda mbele. 

0 maoni:

Chapisha Maoni