Kula mboga za majani zina faida nyingi za kiafya hii ni kutokana na asili yake ya kuwa na:
1. Vitamini kwa wingi
2 . Madini kwa wingi
3. Dawa zinazotokana na mimea kwa kulinda afya.
4. Mboga za majani zinasaidia kukinga mwili kwa magonjwa mbalimbali
5. Mboga za majani pia husadia kupunguza, kurekebisha na kuweka uzito sawa.
Tuangalie sababu kubwa zinazo fanya mboga za majani kupunguza uzito wa mwili ili kuwa na afya bora:
1. Mboga za majani zina mafuta kidogo sana. Mafuta yake yayenyushwa vizuri na joto la mwili kuliko mafuta yatokanayo na mboga za vitoweo vya nyama.
2. Mboga za majani zina nguvu ukaa kidogo sana kulinganisha na mboga zingine kama nyama. Nguvu ukaa zikiwa nyingi mwilini kutokana na chakula zinakuwa mafuta mwilini ambayo unanepa sana na uzito kuongezeka mwilini.
3. Zinaongeza maji kidogo kidogo mwilini kwa sababu mboga za majani zina madini ya sodium kwa wingi.
4. Mboga za majani zinashibisha haraka na kujaza tumbo mapema kwa sababu ya umbirorojo au cellulose
5. Zinaongeza uhai au “vitality” kwa sababu zina virutubisho vingi muhimu kwa mwili.
Kwa hiyo mboga za majani zina sifa zote za kukufanya upunguze uzito kwa zina vitamini nyingi sana na madini ambayo midini ambayo ni muhimu katika kuufanya mwili wako use na afya nyama muda wote.
Pia mboga hii zina kemikali rafiki kwa mwili kwa kuponyesha magonjwa na kuufanya uwe na kinga nzuri sana dhidi ya magonjwa mengi.
Mboga hizi pia hunyonya mafuta toka utumbo mwembamba kwa sababu ya nyunyuzi au umbijani rojorojo au cellulose ambayo zina nyunyuzi kwa wingi. Pia mboga hizi zina mafuta kidogo sana ambayo joto la mwili nyuzi 36.7 centigrade linayeyusha mafuta hiyo kwa urahisi sana.
Mboga hizi pia zina to nguvu ukaa kidogo sana ukilinganisha na vyakula vingine. Mafuta yatokanayo na mboga hawa hayagandi katika damu ndani ya mishipa ya damu tofauti na mafuta yatokanayo na mboga za nyama ambayo husadia katika damu ndani ya mishipa yetu ambayo husababisha vifo vya kushtukiza.
Mafuta ya mboga yanayeyushwa na kuuguzwa kwa hiyo hayakai mwilini katika mfumo wa mafuta “fat”. Mwili unakuwa si wa kunenepa bali unakuwa na afya nzuri yaani mwembamba na mrembo zaidi.
Mboga mboga za majani zina madini muhimu ya sodium kupunguza maji mwilini. Mwili ukiwa na maji mengi unakuwa mnene na mzito kuliko kawaida yake. Kwa hiyo mboga mboga za majani ni muhimu kwa kupunguza maji mwilini na kupunguza uzito.
Mboga mboga hizi zinashibisha mapema na kujaza tumbo ambapo inafanya upate choo vizuri zaidi. Inazuia kuvimbiwa kuliko vyakula vingine. Mwisho katika zinaongeza uhai kwa sababu ya sifa zake. Watu wanaoishi muda mrefu ni wenye kula mboga mboga kwa wingi.
Kula mboga mboga za majani kwa Afya yako
0 maoni:
Chapisha Maoni