Kutoka kulia ni Dk. Zaitun
Bokhary na Dk. Yona Ringo wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
wakimfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo kwenye mfumo wa hewa na chakula
LEO kwa kushirikiana na Profesa Saber M. Waheeb (kushoto) na wenzake
kutoka Misri.
Kutoka kulia ni Dk. Yona Ringo na
Dk. Zaitun Bokhary wa Muhimbili wakiendelea na upasuaji kwa
kushirikiana na wataalamu kutoka Misri.
Profesa Saber M. Waheeb
(katikati) akijadiliana jambo na Dk. Zaitun Bokhary kabla ya kuanza kwa
shughuli ya upasuaji kwa watoto wanane LEO. Kutoka kushoto ni Mwambata
wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na
nchi zote za Mashariki ya kati na Dk Yona Ringo wakifuatilia mazungumzo
hayo LEO.
Grace Joel akiwa na watoto wake
pacha, Eliudi Joel (katikati) na Elikana Joel wakisubiri kufanyiwa
upasuaji wad njia ya mkono. Awali watoto hao kutoka Mbeya walizaliwa
wakiwa wameungana na baadaye walifanyiwa upasuaji na kutenganishwa.
Kutoka kushoto ni Eliudi Joel na
Elikana Joel wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
wakisubiri kufanyiwa upasuaji LEO.
Profesa Dk. Saber M. Waheeb akifanya utafiti mdogo kwa mtoto ambaye amelazwa kwenye Jengo la watoto katika hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kushoto)
akimkaribisha Profesa Saber M. Waheeb katika hospitali hiyo LEO.
Profesa Lawrence Museru (kulia)
akizungumza na madaktari na wataalamu wa kada nyingine LEO katika
hospitali hiyo kabla ya kuanza kwa shughuli ya upasuaji.
Kutoka kushoto ni Mwambata wa
Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanali Salum Haji Othman nchini Misri na
nchi za Mashariki ya kati akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi wa
Huduma za Upasuaji, Dk. Julieth Magandi LEO wa hospitali hiyo.
………………………………………………………………………..
Na John Stephen
Dar es Salaam, Tanzania.
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO imeanza upasuaji kwa watoto
wanane na wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakula
ili kuwa sawa na watu wengine ambao hawana matatizo hayo.
Madaktari wa hospitali hiyo
wanafanya upasuaji huo kwa kushirikiana na madaktari kutoka Misri ambao
wamewasili leo wakitokea Misri kwa ajili ya kushiriki shughuli hiyo.
Madaktari wa Muhimbili ni Dk.
Zaitun Bokhary, Dk. Yona Ringo Madaktari, Dk. Herman Wella, Dk. Victor
Ngolta, Dk Mwajabu Mbaga, Dk. Joachim Angela, Dk. Hashim Lituli na Dk.
Gertrud Mollel wakati madaktari na wataalamu wa kada nyingine kutoka
Misri ni Mahamed Malak, Saber Waheeb, Amr Alaa, Tamer Ghoneim, Ragia
Mohamed Awad, Sherouk Saad Ayoub, Hazem Ahmed.
Wataalamu hao wametembelea
watoto waliolazwa kwenye Jengo la Watoto na kujadiliana na madaktari wa
hospitali hiyo jinsi watakavyotoa huduma za upasuaji kwa watoto hao.
Kwa mujibu wa Dk Julieth
Magandi, watoto wengine sita watafanyiwa upasuaji huo kesho. Dk Magandi
amesema Leo madaktari hao wameanza kwa mtoto mwenye tatizo la mfumo wa
chakula na hewa na kwamba watoto pacha wawili waliungana na
kutenganishwa kutoka Mbeya nao watafanyiwa upasuaji wa kuweka sawa mfumo
wa njia ya mkojo.
Baadhi ya watoto wanaofanyiwa
upasuaji ni; Nasra Rashidi, Hughes Khalid, Fahad Selemani, Elikana Joel,
Eliudi Joel, Hasna Hamis Kalemea, Ibrahim Haji na Sofia Ramadhani.
0 maoni:
Chapisha Maoni