Postedy by Esta Malibiche on August 28.2016 in BIASHARA with No Comment
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akimsikiliza kwa
makini Bi. Rehema Kabuye (katikati) aliyekua akilia kwa uchungu,
akimsihi Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amsaidie ili mume wake ambaye
ni Nahodha wa meli ya MV Liemba pamoja na wafanyakazi wengine wa Mamlaka
ya Huduma za meli mkoani Kigoma, walipwe mishahara yao ya miezi nane
ili kuwaondolea adha ya maisha inayowakabili wao na familia zao
Bi.
Rehema Kabuye, (Katikati) ambaye ni mke wa Nahodha wa Meli ya Mv Liemba,
inayotoa huduma zake Ziwa Tanganyika, akimwonesha Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), picha za mtoto wake ambaye ana
matatizo ya kiafya, akimsihi Waziri huyo amsaidie yeye pamoja na wenzake
ili waume zao walipwe mishahara yao ya miezi 8 wanayomdai mwajiri wao,
Mamlaka ya Huduma za Meli mkoani Kigoma.
Katibu
wa Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Makamba (Kulia), akichukua maelezo
ya kina kutoka kwa Bi. Rehema Kabuye, Mkazi wa Kigoma, ambaye amemwomba
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aingilie kati
sakata la waume zao wanaofanya kazi kwenye mamlaka ya huduma za meli
mkoani Kigoma, ambao hawajalipwa mishahara yao kwa muda mrefu.
Baadhi
ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa
fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), wakati
wa mkutano na Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na
ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF,
mjini Kigoma.
Baadhi
ya wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, wakimsikiliza kwa makini waziri wa
fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango (Mb), wakati wa mkutano na
Waziri huyo kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na ulipaji kodi,
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Baadhi
ya maofisa wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb),
wakati wa mkutano wake na wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), aliyesimama kushoto,
akiwahutubia wafanyabiasha wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali
ya biashara na ulipaji kodi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Katibu
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Kigoma Bw. Raymond Ndabiyegetse
(katikati) akichangia hoja katika kikao na Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) ambaye alipongeza juhudi
zinazofanya na Serikali katika kutengeneza mazingira mazuri ya biashara
zao.
Mkurugenzi
wa kampuni ya Aifola ya Mjini Kigoma, Bw. Zubery Mabie, akiongea kwa
hisia kali akishutumu TRA na maafisa wengine wa serikali katika kituo
kidogo cha Forodha cha Manyovu kilichoko mpakani mwa Tanzania na
Burundi, kujihusisha na rushwa kwa kupitisha maroli yakiwa na mizigo,
ikiwemo chokaa anayozalisha, bila kulipia kodi. Mhe. Dkt. Philip Mpango
(Mb), ameahidi kulifanyiakazi suala hilo.
Mmoja
wa wafanyabiashara wa Mjini Kigoma akichangia hoja katika mkutano
ulioitishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb),
kuhimiza ulipaji kodi, matumizi adili ya fedha za umma, matumizi ya
Mashine za Kieletroniki na utoaji wa risiti, mkutano uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Askofu
Mstaafu wa Kanisa la Anglican, Dkt. Gerard Mpango, akitoa mchango wake
wa mawazo ambapo ameitaka serikali kutoa elimu ya kutosha ya biashara na
ujasiriamali kwa wafanyabiashara nchini ili waweze kutumia fursa
zilizopo katika soko la Afrika Mashariki, kukuza mitaji na biashara zao,
wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na Waziri wa fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), hayupo pichani, uliofanyika katika ukumbi
wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Kamisha
Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, anayeshughulikia masuala ya
kodi, Bw. Shogholo Msangi akifafanua kuhusu kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) kwa wafanyabiashara wa Kigoma Mjini wakati wa mkutano na
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (mb).
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango (Mb), akizungumza na
wafanyabiashara wa Kigoma Mjini, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo
umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya mashine za kieletroniki pamoja na
kuwasisitizia kutoa risiti kwa wateja wao. kushoto kwake ni Kamishna
Msaidizi anayeshughulikia masuala ya kodi, Wizara ya Fedha na Mipango,
Shogholo Msangi, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF,
mjini Kigoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionesha rundo la
makaratasi yaliyoandikwa hoja na kero mbalimbali za wafanyabiashara wa
mjini Kigoma, wakati wa mkutano kati yake na wafanyabiashara hao,
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Askofu Dkt. Gerard Mpango, baada ya kumalizika
kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mjini Kigoma,
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto)
akifurahia jambo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Mhe. Zitto
Kabwe, wakati wakitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa NSSF, ulipofanyika
mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango na wafanyabiashara wa mjini
Kigoma.
Mbunge
wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe (kushoto), akisisitiza jambo wakati
akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Philip Mpango (Mb), baada
ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wafanyabiashara wa mjini Kigoma,
uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NSSF, mjini Kigoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (kushoto) akipeana
mkono na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe, mara baada ya
kumalizika kwa mkutano kati ya Waziri huyo na wafanyabiashara wa Mkoa
wa Kigoma uliofanyika katika ukumbi wa NSSF, mjini Kigoma.
0 maoni:
Chapisha Maoni