Mkurugenzi wa mji wa Kahama,
Andason Msumba akitoa maelezo kwa Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi,
Selemani Jafo kuhusu mgogoro wa soko wanalolitaka wananchi kutumika kwa
maslahi ya wananchi wa mji huo
Naibu waziri Ofisi ya rais,
Tamisemi, Selemani Jafo, akikagua mradi wa maji kijiji cha Chankorongo
wilayani Geita uliohujumiwa na watendaji na kumuagiza Katibu tawala wa
mkoa wa Geita kuunda timu ya uchunguzi.
Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akikagua mashine za kukamulia mafuta ya alizeti mjini Chato.
.
Naibu waziri Ofisi ya rais, Tamisemi, Selemani Jafo, akizungumza na wananchi nje ya kiwanda cha kukamulia alizeti mjini Chato.
……………………………………………………………………….
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais,
Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya
ziara ya Siku mbili katika mikoa ya Shinyanga na Geita na kukagua
miradi mbalimbali.
Akiwa Mkoani Shinyanga, Jafo
alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambapo alijionea changamoto
mbali mbali ikiwepo ya Jengo dogo linalotumiwa na kinamama wakati
wakujifungua kutokana na hospitali hiyo kuzidiwa uwezo.
Kufuatia hali hiyo, Jafo
amemuagiza Injinia wa Wilaya kuhakikisha wanaharakisha ujenzi wa Jengo
kubwa la kisasa la kinamama kwani fedha zipo za Ujenzi huo ili wagonjwa
wasiendelee kupata mateso kwa michakato ya Ujenzi mirefu isiyo na tija.
Kadhalika, akiwa wilayani Kahama,
Naibu Waziri Jafo ametembelea Mradi wa Soko na kumuagiza Mkurugenzi wa
Wilaya, Andason Msumba, kuhakikisha anakaa na timu yake ya Wataalamu ili
kutatua mgogoro wa Soko hilo kwa Maslahi mapana ya wananchi wa Mji wa
Kahama.
Amehitimisha Ziara yake mkoani
Shinyanga kwa kuzungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama na
Halmashauri ya Msalala ambapo amewataka Watumishi kufanya kazi kwa
kujituma huku wakiepuka Uzembe kazini,upendeleo, kupigana majungu, na
kuchukiana.
Katika mkoa wa Geita, Jafo
amekagua mradi wa Maji na Kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeti wilayani
Chato huku akimuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo kuhakikisha
mradi unakamilika mapema kabla ya Mwezi wa 10 ili kuweza kusaidia
kutatua changamoto ya Maji.
Amesema wananchi hawawezi kuwa na Upungufu wa Maji wakati kuna maji mengi ya Ziwa Victoria.
Akikagua Mradi wa kiwanda cha
kukamua Mafuta ya Alizeti, Jafo alimwagiza Mkurugenzi kuhakikisha
anashirikiana na Sido ili kuweza kuukamilisha mradi huo haraka.
Akiwa njiani kuelekea Geita mjini,
Jafo alipita Jimbo la Busanda wilaya ya Geita Vijijini na Kukagua Mradi
wa Maji uliokamilika Kijijini Makondeko kisha Safari ikaelekea Kijiji
cha Chankorongo ambapo kuna Mradi wa Maji wa muda mrefu usio kamilika
ambapo mpaka sasa umetumia zaidi ya Bilioni moja na dalili za kukamilika
bado.
Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri
huyo amemwagiza Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Selestine Gesimba kuunda
tume maalum ya kuchunguza sakata la mradi huo wa maji wa Chankorongo
ambapo wamepewa mwezi mmoja kukamilisha uchunguzi huo.
Alimwagiza Katibu Tawala Mkoa
akishirikiana na Wakurugenzi wote kuhakikisha suara la Oprass linapewa
kipaumbele kwa watumishi na linafanyika kwa wakati na ipasavyo.
Naibu Waziri aliwahakikishia watumishi kuwa serikali inafuatilia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuwataka wawe na Subra.
Wakati huo huo, akiwa Mkoani Geita Jafo alimwakilisha Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika Harambee ya ya kuchangia Madawati.
Katika harambe hiyo Jafo
alihamasisha na kuweza kukusanywa kiasi cha Shilingi Bilioni Moja, mia
saba arobaini Milioni , laki tano na elfu tisini na saba
(1,740,597,000) Kiasi ambacho kilimfanya Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali
Mstaafu Ezekiel Kyunga kumshukuru sana Naibu waziri huyo kwani
hakutegemea kiasi hicho kikubwa cha Fedha kuweza kupatikana.
|
0 maoni:
Chapisha Maoni