Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika kikao maalum
Meneja wa TRA mkoa wa Iringa Joseph Kalinga akizungumza na viongozi wa dini katika kikao maalum |
Viongozi wa dini waliohudhuria kikao wakisikiliza kwa makini
Na Esta Malibiche
Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka viongozi wa
dini mkoani hapa kuwahubiria waumini wao kuhusu wa kulipa kodi kwa kila mfanyabiashara,na
umuhimuwa kudai risiti kwa kila mnunuzi
.
Akizungumza jana katika kikao maalum cha viongozi wa dini
mbalimbali mkoani Iringa , Mkuu wa mkoa alisema kuwa nchi nyingi zilizoendelea duniani,wafanyabiashara wake hawakwepi kulipa kodi,na wanalipa kwa wakati.
‘’’’Ninawaomba viongozi wa dini mkoani hapa kwa pamoja
tushirikiane ili kuwaelimisha wananchi katika vyumba vya ibada na vikao vyetu
tunavyofanya huko,marawanapouza watoe risiti pamoja na wanaponunua wadai risiti
ili kuzuwia ukwepaji wa kulipa kodi’’’
‘’Kama kweli Watanzania tunataka kuyaona mabadiliko
anayofanya mh.Rais kila mfanyabiashara anatakiwa kulipa kodi pasipo kukwepa.Na
mtu yeyote anaekwepa kulipa kodi maana yake huyo mtu ni mwizi.Iko haja ya
kuopambana na wakwepa kodi ili mkoa wetu na Taifa kwa ujumla liweze kusonga
mbele……alisema Masenza
Masenza aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali
kutoa taarifa juu ya wafanyabiashara wasitoa risti baada ya kununua bidhaa.
Aidha mkuu huyo wa mkoa aliitaka TRA kuhajkikisha wanayafikia makundi mbalimbali
wakiwemo waendesha pikipiki [bodaboda] na
kutoa Elimu ya kulipa kodi, ili kila mwananchi aone umuhimu wa kulipa
kodi
‘’Mh .Rais katoa maagizo kutowabughudhi wafanyabiashara
wadogowadogo kama akina mama wanaouza mbogamboga wasilipishwe kodi.Ila wale
wanaosambaza chakula mashuleni ni lazima walipe kodi.Kiongozi yeyote wa dini
asiruhusu mfanyabiashara kusambaza chakula shuleni kwake bila kutoa risiti.’’’
Awali viongozi wa dini walihoji kuhusu TRA walivyojipanga Elimu
kwa mlipa kodi,ambapo Mchungaji Kanani
Baraka za bwana Eliya wa kanisa la Soloam ministry Internation ambae ni mkuu wa
kanisa hilo kanda ya kusini alisema kuwa Elimu ni muhimu sana kutolewa kwa kina
kwa wafanyabiashara ili kila mfanyabiashara anapotoka nyumbani atambue faida
inayotokana na matumizi ya mashine ya kutolea risiti.
Endapo Elimu yenye ufahamu ya kutosha haitatolewa kwa jamii
matokeo yake hakutakuwa na mwamko mkubwa wa wafanyabiashara kuhamasika kununua
mashine hizo na kuzitumia.Pia naomba kuhoji mikakati iliyowekwa na TRA kuhakikisha mashine za EFD zinakuwa na ulinzi
qwa kutosha kutokana na sheria iliyopo kuhusu
usalama wa mtumiaji wa mashine hizo pamoja na uangalizi
utakaosababisha zisichezewe na
matapeli’’’.’’’’’alisema
Sheikh kaimu chalamila
na Abdusalaam Ahamed Ayoub kutoka dhinurey Islam foundation walihoji na kunae kusema
kuwa TRA inatakiwa kuwa na mpango
mahususi kuhakikisha kila mwananchi wa
Iringa atambue kwamba asipopokea risiti ni hatua zipi za kinidhamu zinastahili
achukuliwe,Pia anatakiwa atambue kuwa kutoa
risiti na kutopokea ni jambo la kisheria ambalo limepangwa na serikali
na si vinginevyo
‘’’’Ni muhimu sana TRA watambue ni wanunuzi wangapi
wanofahamyu kwambani lazima kudai risiti baada ya kunu nua.Na niwanunuzi
wangapi wanaofahamu kwamba ukikataa kupokea risitri unaweza kuchukuliwa hatua
gani.’’’’’alisema
Kawa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Iringa Joseph Kalinga akijibu
maswali kutoka kwa viongozi wa dini alisema kuwa adhabu ya mwananchi
atakaeshindwa kudai risiti mara anaponunua vifaa dukani ni Tsh.30,000 kwa
mujibu wa sheria na mwaka 2016 inavyosema na kusisitiza hilo.
Kalinga alisema kwa upande wa Elimu kwa wafanyabiashara
imetolewa vya kutosha kuanzia mjini hadi vijijini
‘’’Tumefanya semina na watu wanaouza vifaa vya
ujenzi,wafanyabiashara wa maduka ya kawaida nay a jumla,kama jitihada hiozo
zimegoma tuna mikakati madhubuti tuliyoipanga kupambana nao.Pia nawaomba
viongozi wetu wa dini tusaidiane kutoa Elimu kwawauminikuhusu kudai risiti na
kutoa risiti ili wafanyabiashara waweze kulipa kodi’’’alisema
Akifafanua kuhusu faida zinazotokana na kutumia mashine za
EFD ,Meneja huyo alisema kuwa,mashine zina
uhakika wa usalama wa taarifa za biashara kutokana na kutunzwa katika
kifaa maalum.Inaahirisha kufanya makadirio sahihi na haki.
Alisema kuwa mashine ni zaidi ya risiti, inaweza kutumika
katika shughuli zingine kama kufanya mauzo na kutuma taarifa mbalimvali,na
zinatoa risiti ambazo ni ngumu kuzigushi.
Aliongeza kuwa lengo la serikali kuwataka wafanyabiashara
watumie mashine hizo ni kuiwezesha serikali
kupanga mipango ya kiuchumi kulingana na mapato ya ndani.Kuimarisha na
kuboresha kumbukumbu za biashara na kutoa haki katika makadilio ya ulipaji kodi
‘’’’’’Kuna sheria mbalimbali za kodi ya ongezeko la thamani
ya 1997,kama ilivyorejewa mwaka 2006.[kanuni za mwaka 2010].Sheria ya kodi ya
mapato ya mwaka 2004,kama ilivyorejewa mwaka 2006[kanuni za mwaka 2012]Pia kuna
sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015[kanuni za mwaka 2016]’’’’’’alisema
MWISHO
0 maoni:
Chapisha Maoni