Alhamisi, 18 Agosti 2016

WANANCHI IPALAMWA KILOLO WAMLILIA MBUNGE KUHUSU KERO YA MAJI



Postedy by Esta Malibiche on August  17.2016 in News
 Wananchi  wa kata ya Ipalamwa wilayani Kilolo wakiwa katika mkutano wahadhara

bamba  hizo  zikitoa maji kama zilizokutwa  leo




Mbunge  wa   jimbo la  Kilolo Venance  Mwamoto  kushoto  akijadiliana jambo  na kaimu  mhandisi  wa maji  wilaya ya  Kilolo  baada ya  kutembelea  mradi wa maji Ipalamwa  ambao wananchi  wanaulalamikia
Tenki la maji mradi ambao  umefadhiliwa na  benki ya  dunia  na kuchangia  na  wananchi zaidi ya Tsh  milioni 9.7  mchango wa  wananchi na mradi  wote  hadi  kukamilika  kwake  utagharimu Tsh  milioni 300


Tenki la maji mradi ambao  umefadhiliwa na  benki ya  dunia  na kuchangia  na  wananchi zaidi ya Tsh  milioni 9.7  mchango wa  wananchi na mradi  wote  hadi  kukamilika  kwake  utagharimu Tsh  milioni 300



WANANCHI  wa  kata ya  Ipalamwa Halmashauri ya  wilaya  ya  Kilolo mkoani  Iringa  wamemlilia  mbunge  wajimbo hilo Kilolo Venance  Mwamoto kutatua kero  ya  maji  ndani ya  mwezi  mmoja  kuanzia  sasa kutokana namradi huo kusuasua kumalizika.

Akizungumza  katika  mkutano  wa hadhara  uliofanyika  katika   viwanja  wa ofisi  ya  Kijiji  cha  Lulindi kata ya  Ipalamwa jana akizungumza kwa niaba ya  wananchi hao  mchungaji  wa kanisa la KKKT, Mkemwa  Bennet  alisema  kuwa kero  kubwa inayowakabili wananchi  ni ukosefu wa maji safi na salama.
  Mbali na kumpongeza  mbunge  Mwamoto  kwa  jitihada  mbali mbali anazozifanya kwa ajili ya  ktatua changamoto za wananchi  wake  wa Kilolo  bado , Mkemwa alisema maji ni kero  ambayo  imekuwa  ikiwatesa wananchi wa vijiji  vya kata  hiyo ya Ipalamwa hivyo alimtaka mbunge huyo kuishughulikia mapema ili wananchi waweze kuondokana na tatizo hilo.

Mkwemwa alisema kuwa huduma  ya  maji  kwenye  kata  hiyo ni changamoto  kubwa japo  kuna mradi  mkubwa wa  maji ulioanzishwa kwa  ufadhili wa benki ya  dunia kati ya  mwaka 2012  ila  hadi  sasa mradi   huo  bado  kukamilika japo huduma ya maji  wamekuwa  wakiipata  kwa mgao.


‘’’Tatizo  kubwa  katika maradi  huo ni bomba ndogo  zilizowekwa ambazo hazimudu kasi kubwa ya maji hivyo mara  kwa mara  bomba  hizo  zimekuwa  zikipasuka na  wananchi  kukosa maji  pamoja na  kuwa mradi   huo hadi  sasa bado  kukabidhiwa  kwa  wananchi ‘’’alisema Mkemwa


Aidha  alimwomba  mbunge  Mwamoto  kusaidia kumaliza kilio  cha  wananchi   cha  kero  ya maji na ikiwezekana ndani ya  mwezi  mmoja kuanzia sasa wananchi  hao hasa wanawake  waondokane na kero ya  maji na  kuelekeza nguvu  zao katika   shughuli za  udhalishaji mali.


Erasto mlengera ni  Mwenyekiti  wa  serikali  ya  kijiji cha  Lulindi alisema  kuwa hadi  sasa mkandarasi  aliyepewa kazi   hiyo ya  kujenga mradi   huo  bado  hajakabidhi mradi kutokana  fedha  alizopaswa  kulipwakutokana na ujenzi huo kutofanyika.
Alisema kiasi cha Tsh milioni 300 fedha  zilizobaki ni chini ya  Tsh  milioni 45 ambazo anadai, hivyo uongozi wa serikali ya  kijiji  wameomba  fedha  hizo zilizobaki asipewe mkandarasi huyo mpaka  mradi   utakapokamilika .

Kwa upande  wake  mbunge Mwamoto  ambae  aliongozana na kaimu mhandisi  wa maji  wilaya ya  Kilolo, aliwaahidi  wananchi hao  kufuatilia ukamilishaji wa maradi  huo  na ndani ya mwezi  mmoja wataoana  mabadiliko katika mradi huo .

Mwamoto alisema iwapo mradi huo utakamilika kwa  ubora  stahiki  wananchi wa kata hiyo wataisahau kero ya maji.
Alisema lengo la  wafadhili  kutoa  fedha  zao na  wananchi  kuchangia kiasi chafedha  ni  kutaka  kuondokana na kero  ya  maji  hivyo haitakuwa busara  kwa viongozi wa  serikali ya  kata  hiyo  kukubali kupokea  mradi ambao haujajengwa  kwa  kiwango .
‘’Nitamfahamisha mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo ,mkuu  wa wilaya ya  Kilolo ambao  wote  ni wageni  ili  kufika  kuona mradi  huu na ikiwezekana  hata  mkuu wa mkoa  wa Iringa nitamuomba kufikahapa,aje ashuhudie hali halisi iliyopo hapa’’’alisema Mwamoto
 Alisema Iwapo mradi  huo hautakamilika kwa wakati kutokana na uzembe unaofanywa na mkandarasi  yeye binafsi hataunga mkono na hatakubali hata  kidogo kuona mkanadarasi akipewa fedha  zilizobaki kabla ya mradi  kujengwa kwa ubora.
MWISHO

0 maoni:

Chapisha Maoni