Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Wilaya
ya Bukombe I liyopo Mkoani Geita sambamba na kukutana na watumishi wa
sekta ya Afya ambapo ametoa maagizo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha
huduma za Afya hapa Nchini.
Akiwa
katika Hospitali ya Wilaya hiyo ya Bukombe, aliweza kubaini mapungufu
mbalimbali ikiwemo jengo la chumba cha Upasuaji ambapo amewaagiza
wafanyie marekebisho ya haraka ili kuiweka katika kiwango cha ubora
unaotakiwa.
Aidha,
ameuagiza uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanafunga mifumo ya malipo
ya kielektroniki na ndani ya miezi sita wawe wanatumia mfumo huo na si
kupokea pesa mkononi.
“Naagiza.
Kuanzia leo ndani ya miezi mitatu muhakikishe mumefunga mfumo wa malipo
kwa njia ya kielekroniki ambapo mfumo huu ufungwe kwenye sehemu zote za
ukusanyaji wa mapato. Mapokezi, Mahabara, Chumba cha X ray, Chumba cha
upasuaji. Hakika ndani ya miezi mitatu mingine muwe tayari mumeachana
na mfumo huu wa kupoea pesa mkononi hivyo baada ya miezi sita mfumo huo
ukamilike na hili ni agizo” alieleza Dk. Kigwangalla.
Dk.
Kigwangalla pia alipata wasaha wa kutembelea kituo cha Afya cha
Ushirombo ambapo ameagiza wahakikishe wanajenga chumba cha Upasuaji
katika moja ya majengo yao ya kituo hicho pamoja na kukarabati vizuri
chumba cha Mahabara ili kutoa huduma bora na zenye uhakika kwa wagonjwa
ambao wamekuwa ni kimbilio kwenye kituo hicho.
Awali
akizungumza na Watumishi wa Idara ya Afya wa Wilaya hiyo, aliwapongeza
kwa kazi za kila siku za kuwatumikia wananchi wa Tanzania ambapo
aliwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano ipo bega kwa began a
inatambua changamoto zao na wanazishughulikia hasa kwa kipindi hiki cha
Hapa Kazi.
“Serikali
inatambua changamoto kwa watumishi wa Afya. Ndio maana hata bajeti ya
mwaka huu ndani ya Wizara yetu imeongezeka mara dufu. Tuwatumikie
wananchi, tufanye kazi kwa moyo na kero na matatizo yote
tunayashughulikia. Sikutaka kukaa Ofisini na kutuma watendaji wa Wizara
bali nakuja mimi mwenyewe kujionea changamoto hizi” alisema Dk.
Kigwangalla.
Hata
hivyo ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Bukombe na Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo kuhakikisha wanashughulikia malipo ya watumishi hao wa
Afya pamoja na watumishi wengine haraka iwezekanovyo kwani imebainika
kuwa, Wao na Madiwani hawana matatizo huku wakilipana stahiki zao kwa
wakati ila watendaji wengine wao wanapata taabu.
Mkuu
wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akizungumza muda mfupi kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amabye alifika kutembelea Hospitali
ya Wilaya ya Bukombe Agosti 20.2016
Baadhi ya watumishi wa Idara ya Afya wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa mkutano huo
Baadhi
ya watumishi mbalimbali wakiwemo wa Afya na Wilaya ya Bukombe
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
Ugeni ukiwasili kwenye kituo cha Afya cha Ushirombo kilichopo Wilayani Bukombe Mkoani Geita.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo ya namna watakavyoboresha kituo hicho
cha Afya kwa upande wa Chumba cha upasuaji na sehemu ya MahabaraNaibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Dk. Kazuzu wa Kituo cha Afya
Ushirombo (kulia) namna atakavyoboresha chumba cha Mahabara na Upasuaji.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo ya Bukombe. DC Maganga.
0 maoni:
Chapisha Maoni