Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiteremka kuelekea eneo la
kuchinjia ng’ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo
Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia
ng’ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro
Agosti 3, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho,
Danstan Mrutu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na
mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro ,
Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) ) wakati walipokitembelea kiwanda
hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watoto
na wananchi wa kijiji cha Majichumvi wilayani Mvomero wakionyesha
mabango wakati WaziriMkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao
kuwasikiliza Agosti 3, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga
wakati alipokagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Morogoro Agosti 3,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Stendi mpya ya mabasi la Msamvu
mjini Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mjini Morogoro baada
ya kukagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Agosti 3, 2016. Kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Stephene Kebwe na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Eliud Sanga. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Awamu
ya kwanza ya jengo la stendi mpya ya mabasi ya Msamvu mjini Morogoro
iliyokamilika kwa asilimia 90. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitembelea
stendi hiyo na kuzungumza na wadau Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza
swali wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya
Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016. Kulia ni
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini
kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na
Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.
Pia aliwataka wafugaji hao
kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo
ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na majosho ili ufugaji wao uwe na
tija.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika
nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Movomero.
Hata hivyo Waziri Mkuu alisema
kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi kitawezesha mifugo yao
kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa ya kutembeza mifugo
umbali mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija ndogo.
Akizungumzia kuhusu uwepo wa
kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri Mkuu alisema
kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa
wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo.
“Uwepo wa viwanda katika maeneo
yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo katika maeneo yetu
ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Viwanda ndiyo
vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati,” alisema.
Kwa upande wake Mkurugenzi na
Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu alisema kiwanda
hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa
siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Desemba mwaka huu.
Mkurugenzi huyo alisema takriban
asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi hasa Uarabuni
kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalum
katika nchi hizo.
“Mbali na uwekezaji huu wa
kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika mnyororo wa thamani
kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi kuzalisha viatu,
mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo
kutoka nje ya nchi,” alisema.
Mrutu alisema nia yao ni kuitikia
wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini
kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani
wataanza kuuza bidhaa hizo.
Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda
hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza majani, mifugo na
mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari wameanza kuhamasisha
jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero, Ngerengere na sehemu
zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero kufanya mapitio ya mashamba ili
kujua wamiliki wake na kama hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka
wa kuyatwaa na kuyarudisha mikononi mwa Serikali.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo
wakati akijibu ujumbe uliokuwa katika mabango yaliyobebwa na wananchi wa
kijiji cha Maji ya Chumvi wilayani Mvomero waliosimamisha msafara
wakati ukitokea kwenye kiwanda cha nyama.
0 maoni:
Chapisha Maoni