Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU wa wilaya
ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,ametoa rai kwa walimu wakuu wa shule za
msingi wilayani humo, kuwafichua walimu walevi kazini na watoro pasipo
kuwalinda ili kulinda nidhamu kazini.
Amesema wapo baadhi ya walimu wanaoshindwa kufuata maadili yao ya kazi ambapo hakuna hatua zinazochukuliwa.
Aidha Assumpter amewataka walimu hao wakuu kuacha kuwaonea haya walimu hao wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kazi.
Alitoa rai hiyo
,wakati alipokuwa anazungumza na walimu wakuu wa shule za msingi
wilayani hapa ,katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya.
Assumpter
aliwaomba wasikubali kukalia tabia hizo ikiwemo kulewa wakati wa kazi
kwani kwa walimu wataoshindwa kuwachukulia hatua wanaojihusisha na
ulevi,utoro wanaweza kujiweka katika mazingira magumu ya kazi.
Aliwaasa walimu kufanya kazi kwa wito, ari na molari ya kazi ili kuinua kiwango cha taaluma wilayani Kibaha.
"Kufanya vibaya
kwa baadhi ya shule ,kunasababishwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
walimu kujiingiza na vitendo vya ulevi na utoro,wanakuwa kikwazo katika
kuendeleza sekta hii muhimu"
"Walimu wakuu
msikubali kuwafumbia macho walimu wa aina hiyo kwani kama mnavyosikia
ngazi za juu wanavyowatumbua, huku nako wasipokuwa makini tusiwafumbie
macho," alisema Assumpter.
Nae afisa
taaluma halmadhauri ya wilaya hiyo, Damas Kimaro alielezea changamoto
ambazo zinasababisha kushuka katika ufaulu kitaifa kutoka nafasi ya 4
mpaka ya 9 imechangiwa na mchakato wa uchaguzi mkuu uliomalizika.
Mwalimu Uhai
Legeza ,alimtaka mkuu huyo atembelee katika shule mbalimbali ili aweze
kujionea namna walimu hao wanavyofanyakazi katika mazingira magumu .
Alisema kuwa
baadhi ya walimu hukaa katika ofisi ambazo hazina thamani bora ikiwemo
viti na meza wanazotumia hazilingani na nyingi hazina ubora.
"Mkuu tembelea katika shule zetu uone viti na meza tunazotumia katika kutimiza majukumu yetu ya kazi," alisema Legeza.
Kufuatia ombi hilo Assumpter aliahidi kutembelea shule hizo kujionea hali hiyo .
Anasema baada
ya serikali kumaliza tatizo la madawati sasa itageukia uboreshaji wa
miundombinu ya majengo ili kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka zaidi.
Mwisho
0 maoni:
Chapisha Maoni