Afisa
Mtendaji wa Millcom Africa Bi Cynthia Gordon akimkabidhi Computer
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma,
anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin,
hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Zanzibar
Afisa
Mtendaji wa Millcom Africa Bi Cynthia Gordon akimkabidhi Computer Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma,
anayeshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin,
Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha na kushoto Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Khadija Juma
Bakari,hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Zanzibar
Maofisa wa Zantel wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhi Computer Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Maofisa wa Zantel wakifuatilia hafla hiyo ya kukabidhi Computer Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Afisa
wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akitowa maelezo wakati wa
hafla hiyo ya kukabidhi Computer Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa
ajili ya matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel Tanzania Benoit Janin
akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Computer kwa ajili ya
Matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika
Ukumbi wa Hotel ya Hyatt Shangani Zanzibar. Na kusema lengo la Zantel ni
kushirikiana na Serikali kwa lengo la kukuza na kuboresha elimu ya
teknolojia na mawasiliano kusaidia vyuo vya Ualimu vinavyotoa Mafunzo
hayoili kuongeza ufanisi
katika ufundidishaji wao..
Afisa
Mtendaji wa Millcom Africa, Bi Cynthia Gordon, akizungumza wakati wa
hafla hiyo na kusema Walimu ndio msingi wa maendeleo kwenye Taifa na
ndio maana Zantel imewapa kipaumbele katika miradi yake ya Kijamii. na
Kusema Zantel Daima imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
tunaboresha sekta elimu kwa wazanzibari na kama tunavyojua elimu ya
teknolojia na mawasiliano ni muhumu kwa dunia ya sasa.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akizungumza
wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Computer na Kampuni ya Simu ya
Zantel kwa ajili ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar hafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa hotel ya Hyatt Shangani Zanzibar, na kuipongeza kampuni
hiyo kwa jitihada zake inayofanya kwa kushirikiana na serikali katika
kukuza na kuboresha elimu visiwani Zanzibar.
‘Ili
kutoa elimu bora kwa walimu wa teknolojia ya mawasiliano wa ngazi zote
ni muhimu kuhakikisha mafunzo ya komputa yanajumuishwa kwenye mtaala wa
vyuo vya elimu ili kuwajengea uwezo walimu katika kufundisha wanafunzi’
Maofisa
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo
ya makabidhiano ya Computer kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Walimu
Zanzibar.
Mkuu
wa Vyo vya Ualimu Zanzibar Maulid Omar Hamad akitowa neno la shukrani
kwa Uongozi wa Zantel Tanzania kwa msaada wao wa Computer 21 kwa ajili
ya matumizi ya Vyo hivyo katika kutowa mafunzo kwa Walimu hao.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma Afisa
wMtendaji Mkuu wa Zantel Benoit Janin.wakifuatilia hafla hiyo
wakimsikiliza Mkuu wa Vyuo vya Walimu akitowa shukrani.
Viongozi
wa meza kuu wakimsikiliza Mkuu wa Vyuo vya Walimu Zanzibar Maulid Omar
Hamad, akitowa shukrani kwa niaba ya Vyuo hivyo wakati wa hafla hiyo ya
kukabidhiwa Computer na Kampuni ya Simu za Mkoni Zantel hafla
iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Zanzibar.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, Mtendaji
Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
Zanzibar Bi Khadija Juma Bakari kushoto Afisa Mtendaji wa Millcom Bi
Cynthia Gordon na Afisa wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha wakiwa
katika picha ya pamoja na Maofisa wa Zantel na Wizara ya Elimu Zanzibar.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amaali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma
akibadilisha mawazo na Mtendaji Mkuu wa Zantel Benoit Janin na Mtendaji
wa Millicom Bi. Cynthia Gordon, baada ya kumalizika kwa hafla ya
kukabidhi Computer kwa ajili ya Matumizi ya Vyuo vya Walimu Zanzibar.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akitowa
shukrani kwa Kampuni ya Zantel kwa msaada wao wa Computer kusaidia
matumizi katika Vyuo vya Walimu Zanzibar. wakati akizungumza na
waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar hafla hiyo
imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Zanzibar.
Mkuu
wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa Baucha akizungumza na Waandishi wa
habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya hafla ya kukabidhi
Computer 21 kwa ajili ya matumizi ya Vyuo vya Ualimu Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni