Na Masanja Mabula –Pemba
WAKATI kampeni ya utoaji wa
Matone ya Vitamin ;A; na Dawa za Minyoo kwa watoto waliochini ya miaka
mitano , likitarajia kufanyika tarehe 23 mwezi huu , uteuzi wa
watendaji kwa ajili ya zoezi hilo umelalamikiwa na baadhi ya masheha wa
Wilaya ya Wete wakidai umefanyika kwa kujuwana .
Wakizungumza na Maofisa wa
Wizara ya Afya Wilaya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Wilaya
hiyo , walisema baadhi watendaji (Cops) wateuliwa bila ya masheha
kushirikishwa jambo ambalo huenda likaleta usumbufu wakati wa zoezi
lenyewe.
Awali Afsa wa Afya Wilaya hiyo
Ali Rashid Said alisema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya kampeni hiyo
yamekamilika ikiwa ni pamoja na vifaa kusambazwa vituoni na watendaji
wakiwa wameandaliwa wamepatiwa mafunzo .
Alisema kila kituo kutakuwa na
wafanyakazi wanne , wawili ni madaktari . mmoja cops pamoja na sheha wa
Shehia husika ambao watashirikiana katika kazi kwa muda wa siku nne .
Sheha wa Shehia ya Fundo Jimbo
la Gando Khamis Abeid alisema COPS walioteuliwa wanaweza kusababisha
kutofanikiwa kwa zoezi hilo , kwani sio ambao walizoeleka kufanya kazi
hizo .
“Cops aliyeteuliwa kufanya kazi
katika Sheha yangu , sio yule wa zamani , na hii inaweza kusababisha
kutofanikiwa kwa zoezi hili , huyo aliyeteuliwa amechaguliwa kwa mtindo
wa kujuwana kwani mimi kama sheha sina taarifa juu ya uteuzi huu
”alieleza.
Naye Sheha wa Shehia ya Bopwe ,
Ramia Said Rashid aliishauri Wizara ya Afya kuacha kuchagua watendaji
amba wanauhusiano nao , bali wawashirikishe masheha kuwapata kwani wapo
waliozoeleka kifanyika kazi hiyo .
Alisema kwamba uteuzi huo
uliofanywa na Wizara ya Afya utazua hisia tofauti kwa wananchi katika
Shehia hiyo na kufahamisha kwamba hatakuwa tayari kubeba lawama ambazo
hasitahili kuzibeba .
Aidha Sheha wa Mtemani Ali Juma
aliutupia lawama Uongozi wa Wizara ya Afya Wilaya hiyo kwa kushindwa
kuwashirikisha katika uteuzi Ili kupata maoni ya masheha kwani Cops
walioachwa wamekuwa wakijitolea kwa kipindi kirefu .
“Kwenye maslahi
hatukushirikishwa , naomba uteuzi huu ukifanyika mara ya pili ni lazima
wawangaliwe na kupewa kipaumbela cops ambao wamefanya kazi siku kwa
njia ya kujitolea ”alishauri .
Katika mazungumzo yake na
masheha afisa wa lishe wilaya hiyo Sabahi Khalfan alisema kwamba tayari
Wizara imeandaa fomu maalumu ambazo Cops wanatakiwa kujaza wakati wa
zoezi la awamu ijayo .
“Ili kuondoa malalamiko ya aina
hii , wizara imeandaa fomu ambao kila cops atajaza , na hii itapunguza
malalamiko , lakini kwa mara hii tunaomba tushirikiane pamoja na ili
tufanikishe kwani hili ni suala la Kitaifa ” alisisitiza.
Aliwaomba masheha kutoa
ushirikiano kwani wanahitaji kupata mafanikio katika zoezi hilo la
kitaifa kwa kuhakikisha wanashiriki kazi ya uhamasishaji ili watoto
waliolengwa waweze kufikishwa vituoni kupata matone na dawa za minyoo .
0 maoni:
Chapisha Maoni