Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inalaani vikali tukio La mauaji ya mtoto
wa kike, umri miaka 9, ambaye alininajisiwa kwa zamu na watu
wasiojulikana, na hatimaye kumkata mapanga yaliyosababisha kuuawa kwa
mtoto huyo mdogo, katika kijiji cha Kapanga, wilaya ya Sumbawanga mkoani
Rukwa.
Wizara imepokea kwa huzuni kubwa
taarifa kuhusu mazingira ya mauaji ya mtoto huyo, ambaye alifanyiwa
ukatili mkubwa yaliyosababisha kifo cha mtoto huyo katika umri mdogo.
Wizara inapongeza agizo la Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima, ambaye amelitaka jeshi la polisi
wilayani Sumbawanga kuhakikisha wanawasaka na kuwatia mbaroni watuhumiwa
wa mauaji ya mtoto ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya
wahusika, na hivyo kuwa fundisho kwa watu wengine.
Wizara inapongeza ushirikiano
uliooneshwa na wakazi wa kijiji cha Kapanga wilayani Sumbawanga, katika
kumtafuta mtoto toka mafichoni kwa ajili ya kuokoa uhai wake. Jitihada
zilizofanywa na jamii ya Kapanga ni uthibitisho kuwa, ulinzi wa mtoto ni
jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.
Kwa niaba ya Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, tunatoa pole kwa marafiki
wa mtoto, wazazi, ndugu na majirani na familia kwa ujumla, na tunawaomba
kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa.
Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
0 maoni:
Chapisha Maoni