Ijumaa, 8 Aprili 2016

Rais Magufuli ashiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji wa Kimbari nchini Rwanda

kiga1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka
22 ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994 ambapo watu takribani milioni
1,000,000 waliuawa.
kiga2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishuhudia  wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame pamoja na binti yao wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo
kiga3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiweka shada la maua wakishuhudiwa na  wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo
kiga4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais Paul Kagame kwa pamoja wakiwasha “Urumuri Rutazima”  (Mwenge/mwali wa Matumaini)  katika maadhimisho Kumbukumbu ya miaka  22 ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo

Maafisa utamaduni wametakiwa kushirikiana na wasanii kuboresha sanaa ili itumike kutangaza maeneo ya utalii wa utamaduni yaliyopo nchini

gei1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wadau wa kada anazozisimamia alipofanya ziara jana Mkoani Geita na kukutana na wadau hao pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa wa Geita. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Manzie Magochie na kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Herman Matemu
gei2
Baadhi ya wadau wa sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na watendaji wa serikali Mkoa wa Geita wakifurahia hotoba iliyotolewa na Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipofanya ziara jana Mkoani Geita kukutana na wadau hao pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari wa mkoa wa Geita.
gei3
: Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya ziwa Eng. Lawi Odiero(aliyesimama) akijibu hoja wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia jana Mkoani Geita. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Manzie Magochie
gei4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (watatu kushoto) akiwasili katika kiwanja cha michezo cha jiji alipofanya ziara jana Mkoani Geita kukutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kuangalia miundombinu ya viwanjwa vya michezo mkoani humo. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Manzie Magochie
gei5
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Geita baada ya kukutana nao jana mkoani hapo na kujadili fursa pamoja na changamoto mbalimbali zinazokabili sekta anazozisimamia. Kulia kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Manzie Magochiena kulia ni Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya ziwa Eng. Lawi Odiero.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Geita
………………………………………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Geita, Maelezo
Maafisa utamaduni nchini wametakiwa kushirikiana na wadau pamoja na kuandaa vikao vya mara kwa mara na wadau wa utamaduni wakiwemo wasanii ili kuweza kujenga ukaribu na kutoa elimu ya sanaa itakayosaidia kuboresha kazi za sanaa hivyo kutumia sanaa kutangaza maeneo ya utalii wa utamaduni yaliyopo nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia pamoja na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari jana Mkoani Geita.
Mhe. Nnauye amesema kuwa kama maafisa utamaduni watakua karibu na wadau wa sanaa na utamaduni ujuzi wa tasnia ya sanaa na utamaduni utaongezeka kwa kujifunza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine hivyo kukuza vipaji vya wasanii vitakavyotumika kutangaza maeneo ya utalii wa utamaduni na kuvutia watalii pamoja na wawekezaji.
Aidha Mhe. Nnauye ameitaka jamii kuheshimu kazi za sanaa na kuwathamini wasanii kwani serikali inampango wa kurasimisha kazi za sanaa hivyo kuifanya sanaa kuwa  shughuli rasmi ya kiuchumi itakayowawezesha wawekezaji kuwekeza katika sanaa na kumfanya msanii apate kipato kizuri lakini pia kuiwezesha serikali kupata kipato kupitia tasnia ya sanaa na utamaduni.
Naye Mwenyekiti wa chama cha Waigizaji Mkoa wa Geita Bibi. Rosemery Michael amemuomba Mhe. Waziri kuhakikisha kuwa wasanii wanapata usajili na kuwa na uhalali wa kufanya kazi zao kwa kuhakikisha kuwa wasanii wanafuata sheria na taratibu zitakazowapa muongozo wa kufanya shughuli zao kwa ufanisi na weledi hivyo kuwaongezea kipato.
Bibi. Michael amesema kuwa tasnia ya sanaa inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutokuwa na chuo cha sanaa mikoani, wasanii kutokua na elimu ya sanaa itakayowajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi, wasanii kufanya kazi kiholela, pamoja na uhaba wa uwekezaji katika tasnia ya sanaa.
Aidha Katibu wa Chama cha waigizaji Mkoa wa Geita Bw. Kangeta Ismaili ameomba mfuko wa maendeleo ya vijana kutambua vikundi vya wasanii na kuvifikia vikundi hivyo kwa kuwapa mikopo ambayo itawawezesha kuboresha kazi za sanaa na kuwainua wasanii kiuchumi.

0 maoni:

Chapisha Maoni