Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha linakabidhi
kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando ifikapo Aprili 25,
2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho bwana Justine Eminoga ambacho
amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara wa Jijini humo kwa zaidi ya
miaka sita sasa.
Mongella amefikia hatua hiyo mara
baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana Justine ambaye alifika
katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake ambalo limedumu kwa
zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa
mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara
aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Kwimba.
Katika hatua nyingine mkuu huyo
wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha
wanakamilisha zoezi la kuhakiki watumishi, ili kubaini endapo kuna
watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo
linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kamati
maalumu zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo,
Akiwa katika ziara hiyo mkuu huyo
wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa Utumishi msaidizi wa jiji la
Mwanza Henry Sedetale, ambaye alisaidia watumishi hewa watano kuchukua
mikopo ya zaidi ya Mil.90 kutoka katika benki tofauti tofauti, hata
hivyo taarifa kutoka Taasisi yakupambana na kuzuia rushwa mkoani
Mwanza iliyotolewa wakati wa kikao hicho na mkuu wa Takukuru mkoani
humo, ilisema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa ametiwa nguvuni na taasisi
hiyo kwa mahojiano zaidi.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza yupo
katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na hii ikiwa ni Wilaya yake
ya tatu mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi na Magu hapo awali.
Imetolewa na
Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA MAHUSIANO –RS MWANZA. 18 Aprili, 2016
0 maoni:
Chapisha Maoni