Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Ravia Idarous Faina wa
kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) katika
uchaguzi ulifanyika jana katika ukumbi wa Uwanja wa Gombani, Pemba.
Katika salamu zake, Malinzi
amesema anampongeza Ravia kwa kuchaguliwa kwake, na hiyo imeonyesha
imani kubwa kwa waliomchagua kuongoza ZFA katika kipindi kingine.
Malinzi amewapongeza vingozi wote
wapya waliochaguliwa katika uchaguzi huo, na kuahidi kuendelea
kushirikiana nao katika shughuli zote za maendeleo ya mpira wa miguu.
Uchaguzi wa kupata viongozi wa
ZFA ulifanyika jana Gombani kisiwani Pemba, ambapo Ravia aliibuka
mshindi na kutetea nafasi yake, nafasi ya makamu wa rais Ugunja kienda
kwa Mzee Zam Ali, na makamu wa Pemba ikichukuliwa na Ali Mohamed Ali.
0 maoni:
Chapisha Maoni