Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika
viwanja mbalimbali nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo
hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
Jumamosi, Young Africans watakua
wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
huku Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja
wa Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.
Coastal Union watawakaribisha
maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku
Jumapili, Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni